Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Wateja Wengi Wananunua Kwa Watu Hawa Hapa

Binadamu ni viumbe vya hisia na siyo maroboti.

Kabla hatujaendelea, naomba ujiulize swali hili. Mauzo mengi unayofanya huwa unanunua kwa watu wa aina gani?

Habari njema ni kwamba vitu vingi tunavyonunua tunanunua kwa watu tunaowapenda. Na watu huwa wananunua kwa watu wanaowapenda.

Watu hawanunui kwa watu wanaowachukia. Mauzo mengi ambayo wateja wanayafanya, wanafanya kwa wale ambao wanawapenda.

Sina uhakika kama itakufaa lakini unaona nguvu ya mahusiano ilivyokuwa kubwa?ndiyo maana tunasema mauzo ni mahusiano. Na habari njema ni kwamba kitabu chako MAUZO NI MAHUSIANO kipo tayari na kinapatikana kwa shilingi elfu 20 tu.

Mauzo ni mahusiano kwa sababu watu wananunua kwa watu wanaowapenda. Mara nyingi tunajisikia vizuri pale tunaponunua kwa watu tunaowapenda.

Wewe chunguza tu, utaona mambo mengi tunayofanya au manunuzi huwa tunafanya kwa yule ambaye tunampenda. Mtu ambaye hatumpendi wala huwa hajisumbui kununua kwake.

Mpaka unaona tunanunua kwa mtu, basi jua tunampenda lakini pia tuna mahusiano mazuri naye. Kama hatuna mahusiano mazuri na wateja wetu basi ni ngumu kufanya mauzo.

Kazi ya mauzo inakuwa rahisi pale ambapo tunakuwa na mahusiano mazuri na wateja wetu. Tukiwapenda wateja wetu basi watajisikia vizuri na wakijisikia vizuri watakuja kununua kwetu.

Wateja wetu wakitupenda watatupa dili nzuri. Siyo tu dili nzuri lakini pia watatupa koneksheni mbalimbali.

Hatua ya kuchukua leo; wapende wateja wako kwa sababu watu wananunua kwa watu wanaowapenda.
Tengeneza mahusiano mazuri na wateja wako.

Kitu kimoja zaidi, pata kitabu chako cha MAUZO NI MAHUSIANO ili kikusaidie kupata mbinu za kujenga mahusiano bora na wateja wako na kuwafanya kuwa wako daima.

Na ukiwafanya wateja wako kuwa kwako daima maana yake mauzo kwako siyo tatizo tena. Narudia tena, kama bado hujasoma kitabu cha MAUZO NI MAHUSIANO, piga hii namba 0717101505 sema uko wapi utatumiwa kitabu chako.
Watu wengi wameshapata nakala zao kama na wewe bado fanya fasta upate yako kabla hazijaisha.

Kutoka kwa rafiki na muuzaji mwenzako,
CIO, Mwl Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa Chuo Cha Mauzo,
Barua pepe; makamu@mauzo.tz
Simu; 0717101505 wasapu na kawaida/0767101504.
http://www.t.me/chuochamauzo
www.mauzo.tz

Leave a comment