Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Umuhimu Wa Kukaa Katika Eneo La Biashara Muda Mwingi

Pata picha ni asubuhi na mapema umechemsha maji kwa ajili ya chai au umepika chai. Kwa bahati mbaya ukakuta sukari, majani au mkate umeisha.

Ukawaza mtaani kwako, kuna duka linafunguliwa mapema sana. Hivyo, ukamua kwenda katika duka hilo. Kwa ajili ya kuchukua budhaa. Ile unafika tu, duka limefungwa. Utajisikiaje? Utaumia sana na kuona kama muuzaji wa duka amepoteza muda wako.

Wakati unawaza, kwa mbali ukaona duka lingine limefungliwa haraka sana ukaenda kuchukua bidhaa pale. Je, kesho asubuhi ukihitaji bidhaa ni duka lipi utaliwaza kikiwa la kwanza? Jibu itakuwa ni duka la pili. Kwa sababu maumivu ya kukuta limefungwa Jana ni makubwa. Kuna namna umekuwa “disappointed”.

Mfano mwingine, imefika muda wa taarifa ya habari ukawasha TV yako. Ile unawasha tu, uangalie taarifa ya habari hukuti mtangazaji hata mmoja, ile channel uliyoitegemea ukakuta inaonyesha muziki utajisikiaje? Jibu ni vibaya. Lakini kwa kuwa kila wakati watangazaji wa TV wapo kazini mara zote. Unakuwa huna wasi wasi wowote muda wa kuangalia taarifa ya habari unapowadia.

Au kuna wakati unapiga simu kwenye mtandao mojawapo inawachukua muda mrefu kukuhudumia. Sio kwamba hawapokei ila unapewa taarifa kuwa wanawahudumia wateja wengine. Unaanza kujawa na hasira. Unawaza namna wanavyochukulia. Pengine unaanza kulalamika huduma za mtandao fulani mbaya. Hawapokei wateja kwa wakati. Namna unavyolalamika na kujisikia, ndivyo wateja wako wanajisikia ikiwa hujawa na utayari kuwapokea kwa wakati.

Hivi ndivyo wateja wanavyojisikia wanapofika katika eneo letu la biashara na kukuta tumefunga. Wanaumia na wanaanza kukosa imani na sisi.

Kwa hiyo uwepo wako katika eneo la biashara ni kitu muhimu sana katika kutoa huduma nzuri. Maana wateja mara zote wanahitaji kupata huduma kwa mtu ambaye anaweza kupatikana mara nyingi zaidi. Ikiwa unatoa huduma kwa kusua sua mara upo kesho haupo katika biashara unawakatisha tamaa. Hali inayowafanya wanaamua kwenda sehemu wanayopata huduma mara tu baada ya kuihitaji.

Mambo machache ya kuzingatia ili kukaa katika eneo la biashara;

Moja; Ijue kwa nini ya kuanzisha biashara
Mbili; Tunza taarifa za wateja wako
Tatu; Weka fokasi kwenye malengo ya biashara yako
Nne; Kuwa mvumilivu

Umuhimu wa kuwa eneo la biashara;

Moja; Unaaminika mbele ya wateja

Mbili; Unategemewa na wateja

Tatu; Unafikiriwa na wateja wako

Jitahidi ufanyie kazi yote uliyojifunza katika somo hili.

Imeandaliwa na Lackius Robert, Mkufunzi Msaidizi wa Chuo Cha Mauzo. Tuwasiliane 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz

1 Comment

  • Miraji abdallah
    Posted January 26, 2024 at 11:20 am

    Ili biashara yangu iweze kufanikiwa, ninapaswa kukaa tkt biashara yangu muda mwingi. Kwa kufanya hivyo wateja watanitegemea, kuniamini pia watakapokua na uhitaji watanikimbuka .
    Asante MKUFUNZI LACKUS ROBERT

Leave a comment