Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Mbinu Mbili Za Ukamilishaji Wa Mauzo 13-14

Rafiki,
Kwenye mauzo, huwa tuna mchakato wa kuwatafuta wateja wapya, halafu tunawashawishi kununua, sasa kitendo cha kuwashawishi wateja na kununua ndiyo tunakiita ukamilishaji.

Wauzaji wengi wanakuwa wanawaelezea wateja kile wanachouza, wanapofikia kwenye ukamilishaji wanakuwa wanakubali kirahisi sababu wanazopewa na wateja na hivyo kushindwa kukamilisha mauzo.

Sababu kama vile ngoja niende nitarudi, nitakuja nikiwa tayari, Sina fedha, ngoja nizungukezunguke Kwanza, nitakutafuta nikiwa tayari.
Ngoja nikaongee na mume au mke au ngoja nikafikirie kwanza.

Na mara nyingi wateja huwa wanadanganya, hata kama kitu hakitaki kweli, hawezi kukuambia ukweli Bali atakumbia sababu zao nzuri Kama nitakutafuta nikiwa tayari na wewe ukimkubalia basi hiyo ndiyo inakua imeisha harudi Tena.
Kwa asili, mteja anaogopa kukuambia hataki, anajua atakuumiza hivyo anakutafutia pingamizi moja zuri au sababu ambayo akikuambia utamwamini na yeye kuendelea na vitu vingine.

Na kwa kipindi hiki, sababu ni januari ni ngumu, mvua, ada, nk kwa hiyo ukiambiwa tu, unaridhika. Siyo kwamba wateja wanakuwa hawana hela, wanazo ila wanahitaji Kwanza uweze kuibua maumivu yao , uwashawishi kwenye kile unachouza kwamba hawawezi kuendelea kuishi bila kuwa na kile unachouza. Uibue tamaa ndiyo watashawishika kununua.

Kwenye kanuni ya soko kubwa, ni asilimia 3 tu ya walio tayari kununua na wengine wote wanahitaji ushawishi.
Asilimia 17, ni wateja ambao wanakusanya taarifa.
20% wanaojua wana tatizo. Na asilimia 60 wasiojua kama wana tatizo.
Hivyo unahitaji ushawishi kuweza kuwaonesha watu ambao wanaishi na kujiona hawana matatizo kumbe wanayo. Mfano, ukimwambia mtu unauza dawa za presha hawezi kushawishika kununua ,lakini ukimpima presha na vipimo vikaonesha kuwa ana tatizo, hawezi kuacha kununua, lakini ukimshawishi bila kuibua tatizo hawezi kununua.

Wateja hawataki kujitenganisha na fedha zao, wewe kama muuzaji bora kuwahi kutokea hupaswi kukubaliana na kile mteja anachokuambia.
Ni wajibu wako kabisa wa kimaadili kuhakikisha mteja anapata kile unachouza kwa sababu kina manufaa kwake.
Hivyo tunapaswa kutumia kina aina ya mbinu kuwashawishi wateja kununua.

Leo tunakwenda kujifunza mbinu mbili za uhakika kabisa za ukamilishaji wa mauzo.
Na habari njema ni kwamba leo tujifunza mbinu namba 13-14

  1. Ukamilishaji wa mshauri.
    Mnunuaji anaweza akaambatana na mshauri na huyo mshauri akawa ni mjuaji anamshauri labda hiyo siyo sawa. Kila kitu anamuuliza mshauri unaonaje kwenye hili?
    Sasa unapaswa kumleta huyo mshauri upande wako, kwa mfano, John, kwa hii bei, ukizingatia vile unavyoijua hii bidhaa na unavyomjua ndugu/rafiki yako, unaweza kumshauri nini kuhusu bidhaa hii na usawa wa bei?
    Hapa unakuwa unamvuta na kumtambua kwamba yeye ni mtaalamu na atapata kichwa, kwa jinsi unavyomjua huyu rafiki au ndugu yako, unamshauri nini kwenye hili. Atajitahidi amshauri aliyeambatana naye kwa sababu tayari umemfanya yeye ni mtaalamu hivyo atamshawishi anunue.

Huu ni ukamilishaji wa kutumia pale mnunuaji anapokuwa ameambatana na mtu wa kumshauri kwenye manunuzi.
Mhusishe mtu huyo kwa sababu mnunuaji anamsikiliza zaidi na kumwamini.
Kitendo cha kumshawishi mshauri kukubali, unakuwa umemshawishi mteja kukubali pia.

  1. Ukamilishaji wa anayeambatana naye -1

Wakati mwingine mteja anakuwa ameambatana na mtu na ana nguvu sana mtu huyo na wewe unaona kama vile jamaa anataka kukuharibia dili kwa mteja wako.
Sasa ili kumkata nguvu, unamuuliza tu kwa upole, kwenye haya manunuzi wewe utasaidia kwenye bei, malipo, usajili au vyote?
Kama atakua hana cha kuchangia atakuachia nafasi ya wewe kukamilisha manunuzi na mteja wako na unamuuliza kwa lugha ya upole na upendo.

Huu ni ukamilishaji wa kutumia kwa mtu anayeambatana na mnunuaji, anayeonekana kuongea sana ila hujui nafasi yake kwenye manunuzi ni ipi.
Kwa muuliza hivyo, itamfanya aeleze nafasi yake ni ipi au anyamaze kama hahusiki moja kwa moja.

Hatua ya kuchukua leo; nenda kazitumie mbinu hizi mbili ulizojifunza leo kwa vitendo na kisha ujue utupatie ushuhuda wiki ijayo.

Mwl.Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz

Leave a comment