Showing 14 Result(s)

Wateja Wengi Wananunua Kwa Watu Hawa Hapa

Binadamu ni viumbe vya hisia na siyo maroboti. Kabla hatujaendelea, naomba ujiulize swali hili. Mauzo mengi unayofanya huwa unanunua kwa watu wa aina gani? Habari njema ni kwamba vitu vingi tunavyonunua tunanunua kwa watu tunaowapenda. Na watu huwa wananunua kwa watu wanaowapenda. Watu hawanunui kwa watu wanaowachukia. Mauzo mengi ambayo wateja wanayafanya, wanafanya kwa wale …

Zana Yenye Nguvu Katika Kukuza Mauzo Yako Mara Mbili na Zaidi

Umewahi kufikiria ni kwa namna gani simu yako inaweza kukunufaisha zaidi? Ndiyo! Simu yako inaweza kufanya mambo mengi zaidi unavyofikiria. Songa nami upate dondoo zinazoenda kukusaidia kukuza mauzo yako mara mbili zaidi na kuboresha maisha yako. Ndugu, Simu ni zana bora na itaendelea kuwa zana bora na yenye nguvu zaidi kwenye mauzo. Ilianza kuwa na …

Jinsi Ya Kuongeza Mauzo

Habari njema ni kwamba, kila mtu anapenda kupata faida. Kila mtu anapenda kuongeza mauzo kama anafanya biashara. Kila mtu anapenda kupata matokeo mazuri zaidi. Na mauzo ndiyo moyo wa biashara. Kwa sababu, kupitia mauzo kila kitu kinapatikana. Kama mauzo yakiongezeka, utapata mapato makubwa, utajilipa vizuri, utawalipa wasaidizi wako vizuri.Utafanya maendeleo kwenye biashara yako. Wote tunajua …

Hivi ndivyo unavyoenda kumbakiza mteja katika biashara yako.

Ndugu, Natumaini umewahi kununua viatu, nguo au mahitaji madogo madogo ya nyumbani kama vile sukari, chumvi au chakula. Je, ulipomaliza kutumia mahitaji hayo, ulikuwa ni mwisho wa maisha yako? Jibu ni hapana. Uliendelea kuyanunua tena na tena, maana ni muhimu katika kuendesha maisha yako. Kwa kuwa ni muhimu, basi kuna sehemu unaenda mara nyingi kuchukua …

Sehemu Pekee Unayopaswa Kuanza Nayo Kama Unataka Kuuza Sana

Mpendwa muuzaji, Hakuna zama ambazo ni rahisi kuuza kama zama hizi tunazoishi sasa. Kama huuzi katika zama hizi na una huduma nzuri au bidhaa basi hiyo ni shida yako binafsi. Hii ni kama vile unakufa na kiu, wakati uko kisimani. Kama unasoma hapa, halafu unahangaika huuzi, basi utakua unajipunja sana. Habari njema ni kwamba, ukiwa …

Siri kuu ya mauzo inayoenda kukuletea wateja wengi zaidi wa uhakika

Ndugu yangu, Unakumbuka siku ulipopata changamoto, ukaenda Kwa rafiki yako kumwomba msaada? Mara baada ya kukusaidia kupata utatuzi wa changamoto yako ukifurahia sana. Kila mara unapomuona unajisikia vizuri, ikiwa akiomba kitu ni rahisi kumsaidia maana aliwahi kukusaidia. Kumbe, msaada ni kitu kinachotolewa kwa mtu mwenye shida ili kuiondoa au kutimiza haja yake. Sisi binadamu huwa …

Jinsi Ya Kuimarisha Mahusiano Na Wateja Wako

Kwenye maisha siri ya kupata ni kutoa. Mafanikio yoyote duniani yanakuja kwa njia ya kutoa. Huwezi kupata kile unachotaka kama hujatoa. Ukitaka kitu ambacho huna unatoa hela na hela inakusaidia kupata kile unachotaka kwenye maisha yako. Kama unataka ng’ombe wako atoe maziwa mengi, basi mshibishe vizuri na utapata maziwa mengi. Kwa chochote kile unachotaka kupokea, …

Hivi ndivyo unavyoenda kuwafanya wateja waipende biashara yako

Watu wanaweza kuwa wanakaa sehemu moja lakini hawanunui kwao. Sio kwamba bidhaa hamna wala biashara kufunguliwa ila ni namna tu ya huduma wanayopewa. Ikiwa wanahudumiwa vizuri ni rahisi kurudi kila mara tofauti na wanapohudumiwa vibaya. Pata picha umeenda kupata huduma fulani, ukaelezea unachotaka mhudumiaji anakutazama tu. Huku muda ukiwa unaenda, lakini wengine wanahudumiwa. Je, utafurahia …

Jinsi Ya Kupata Wateja Wanaoaminika

Mpendwa muuzaji bora kuwahi kutokea, Kila mmoja wetu anapenda kupata wateja wazuri na wanaoaminika. Kazi yako kubwa kama muuzaji ni kujenga wateja wanaoaminika kwenye biashara. Ili uweze kupata wateja wanaoaminika kwenye biashara yako, unapaswa kwanza wewe jenga kujenga kuaminika kwa wateja wako. Huwezi kujenga wateja wanaoaminika kama wewe mwenyewe hujaaminika. Jenga kuaminika, wafanye watu wakutegemee …

Jinsi ya kumuuzia mteja kwa urahisi na haraka

Je, wajua kuwa, unaweza kumuuzia mteja kwa urahisi na haraka? Fuatilia somo hili utapata mbinu zaidi; Maria na Jenifer wanauza duka katika eneo A. Wote wanauza bidhaa zinazofanana. Yaani; Rosheni, mikoba na pochi za wanawake. Bei zao hazitofautiani, maana wote “Supplier” wao ni mmoja. Maria anauza zaidi kuliko Jenifer. Kila unapofika mwisho wa mwezi na …