Karibu CHUO CHA MAUZO.

CHUO CHA MAUZO ni programu ya mafunzo kwa watu wa mauzo yenye lengo la kuwafanya kuwa wauzaji bora. Ni programu yenye mafunzo ya nadharia na vitendo ambayo yanagusa maeneo yote muhimu ya mauzo ili kumjengea muuzaji ujuzi bora wa mauzo utakaomwezesha kufanya mauzo makubwa. Programu hii ina urefu wa mwaka mmoja (wiki 50) ambapo kuna …

Hivi ndivyo unavyoenda kumbakiza mteja katika biashara yako.

Ndugu, Natumaini umewahi kununua viatu, nguo au mahitaji madogo madogo ya nyumbani kama vile sukari, chumvi au chakula. Je, ulipomaliza kutumia mahitaji hayo, ulikuwa ni mwisho wa maisha yako? Jibu ni hapana. Uliendelea kuyanunua tena na tena, maana ni muhimu katika kuendesha maisha yako. Kwa kuwa ni muhimu, basi kuna sehemu unaenda mara nyingi kuchukua …

Sehemu Pekee Unayopaswa Kuanza Nayo Kama Unataka Kuuza Sana

Mpendwa muuzaji, Hakuna zama ambazo ni rahisi kuuza kama zama hizi tunazoishi sasa. Kama huuzi katika zama hizi na una huduma nzuri au bidhaa basi hiyo ni shida yako binafsi. Hii ni kama vile unakufa na kiu, wakati uko kisimani. Kama unasoma hapa, halafu unahangaika huuzi, basi utakua unajipunja sana. Habari njema ni kwamba, ukiwa …

Siri kuu ya mauzo inayoenda kukuletea wateja wengi zaidi wa uhakika

Ndugu yangu, Unakumbuka siku ulipopata changamoto, ukaenda Kwa rafiki yako kumwomba msaada? Mara baada ya kukusaidia kupata utatuzi wa changamoto yako ukifurahia sana. Kila mara unapomuona unajisikia vizuri, ikiwa akiomba kitu ni rahisi kumsaidia maana aliwahi kukusaidia. Kumbe, msaada ni kitu kinachotolewa kwa mtu mwenye shida ili kuiondoa au kutimiza haja yake. Sisi binadamu huwa …

Jinsi Ya Kuimarisha Mahusiano Na Wateja Wako

Kwenye maisha siri ya kupata ni kutoa. Mafanikio yoyote duniani yanakuja kwa njia ya kutoa. Huwezi kupata kile unachotaka kama hujatoa. Ukitaka kitu ambacho huna unatoa hela na hela inakusaidia kupata kile unachotaka kwenye maisha yako. Kama unataka ng’ombe wako atoe maziwa mengi, basi mshibishe vizuri na utapata maziwa mengi. Kwa chochote kile unachotaka kupokea, …

Hivi ndivyo unavyoenda kuwafanya wateja waipende biashara yako

Watu wanaweza kuwa wanakaa sehemu moja lakini hawanunui kwao. Sio kwamba bidhaa hamna wala biashara kufunguliwa ila ni namna tu ya huduma wanayopewa. Ikiwa wanahudumiwa vizuri ni rahisi kurudi kila mara tofauti na wanapohudumiwa vibaya. Pata picha umeenda kupata huduma fulani, ukaelezea unachotaka mhudumiaji anakutazama tu. Huku muda ukiwa unaenda, lakini wengine wanahudumiwa. Je, utafurahia …

Jinsi Ya Kupata Wateja Wanaoaminika

Mpendwa muuzaji bora kuwahi kutokea, Kila mmoja wetu anapenda kupata wateja wazuri na wanaoaminika. Kazi yako kubwa kama muuzaji ni kujenga wateja wanaoaminika kwenye biashara. Ili uweze kupata wateja wanaoaminika kwenye biashara yako, unapaswa kwanza wewe jenga kujenga kuaminika kwa wateja wako. Huwezi kujenga wateja wanaoaminika kama wewe mwenyewe hujaaminika. Jenga kuaminika, wafanye watu wakutegemee …

Jinsi ya kumuuzia mteja kwa urahisi na haraka

Je, wajua kuwa, unaweza kumuuzia mteja kwa urahisi na haraka? Fuatilia somo hili utapata mbinu zaidi; Maria na Jenifer wanauza duka katika eneo A. Wote wanauza bidhaa zinazofanana. Yaani; Rosheni, mikoba na pochi za wanawake. Bei zao hazitofautiani, maana wote “Supplier” wao ni mmoja. Maria anauza zaidi kuliko Jenifer. Kila unapofika mwisho wa mwezi na …

Kifaa Kinachotuunganisha Katika Kujenga Mahusiano Na Wateja

Pata picha una mpenzi wako ambaye yuko Iringa na wewe uko Dar na kuonana na mpenzi wako ni mpaka wakati wa likizo tu.Utajisikiaje kukaa na mpenzi wako kwa muda mrefu hivyo bila kuwasiliana naye mpaka mje kuonana wakati wa likizo? Na kama unavyojua, ni hali ya hatari sana kwa mtu ambaye mnahusiana katika mapenzi halafu …

Jinsi ya kumjua mteja na kumuhudumia zaidi

Habari za leo ndugu yangu mpendwa? Naamini umewahi kuona nyumba ikiungua moto, simu ikiishiwa vocha, nguo ikichanika, Kingamuzi kikiishiwa kifurushi, maji yakikatika au gari likiishiwa mafuta. Ni hali za kawaida kutokea katika maisha yetu. Je, nyumba ilipoungua ulienda kwa nani kupata usaidizi? Simu ilipoishiwa vocha ulienda kununua wapi? Nguo ilipochanika ulienda kwa nani ili kuirekebisha? …

Jinsi Ya Kupata Wateja Wengi Na Endelevu Kwenye Biashara Yako

Pata picha unatoka zako nyumbani, uko zako kwenye mishe mishe zako mara ghafla unakutana na mwanamke au mwanaume anakusalimia na kukuambia nimekupenda naomba nikuoe au unioe kwa mara ya kwanza tu na hamjawahi kuonana hata siku moja utajisikiaje kwa mfano? Utamshangaa! vipi huyu kaka au dada amechanganyikiwa nini? Au atakua ana wazimu? Au wewe ni …