Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Mbinu Mbili Za Ukamilishaji Wa Mauzo 8-9

Habari njema wauzaji bora kuwahi kutokea,

Wewe kama muuzaji, mara zote unapaswa kukamilisha wateja.
Ni katika kukamilisha wateja, na kununua ndiyo fedha inaingia kwenye biashara.
Mchezo wowote ule, raha yake ni ushindi.

Hivyo basi, kila wakati kuwa na njaa ya kuuza, uza kama chizi na utapata matokeo mazuri.

Leo kwenye jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo na leo tunaendelea na mbinu namba 8 na 9.

8. Ukamilishaji wa kuongea na mwenza – 2.

Pale unapokutana na mteja, na anakuambia pingamizi la mwenza ambalo  linakuzuia wewe usikamilishe mauzo unapaswa kumuuliza hivi;

(Anasema anahitaji kuongea na mwenza wake kwanza) “Nakubaliana na wewe na ni vizuri kufanya hivyo, lakini kama mwenza wako yupo kama wangu, huwa hanikatalii kwenye kitu ambacho nakipenda kweli, na mimi pia huwa simkatalii kwenye vitu anavyopenda.
Weka sahihi yako hapa …kama biashara inahusisha sahihi.
Kama haihusishi sahihi, mwambie tukamilishe hili, na kinachofuata baada ya hapa ni wewe kulipia bidhaa yako ili uweze kuondoka nayo.

Ufafanuzi; ukamilishaji huu unapaswa kutumiwa kwa kujiamini na kwa haraka na uimara. Unakubaliana naye, unatabasamu na kumweleza upande wako, na hilo linamfanya akose sababu ya kupinga.

9. Ukamilishaji wa kuongea na mwenza – 3.

Unamshawishi mteja akamilishe malipo, anakuambia nahitaji kuongea na mwenza unapaswa kutumia mbinu hii ya ukamilishaji wa malipo.
(Anasema anahitaji kuongea na mwenza wake kwanza) unamwambia mteja,  “Ni bora kuomba msamaha kuliko kuomba ruhusa, ruhusa inaweza kukataliwa, lakini msamaha mara zote hukubaliwa. Tufanye maamuzi sasa, weka sahihi yako hapa au chukua bidhaa na lipia sasa uende ukaifurahie.

Ufafanuzi; huu ni ukamilishaji wa juu na unaohitaji ubobezi na mamlaka wakati unatumia. Hivyo mwangalie mtu machoni na tabasamu wakati unamwambia.

Hatua ya kuchukua leo; tumia ukamilishaji huu leo kwa vitendo ili uweze kupata matokeo.
Usikubali mteja aseme ngoja akawasiliane na mwenza kwanza wakati tayari una mbinu hapa.

Mwl.Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz

Leave a comment