Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Mjue Mteja Tarajiwa Ili Ukuze Mauzo Yako

Mteja Tarajiwa, huyu ni mteja uliyemfikia kwa njia ya simu au usakaji au aliyekutafuta kwa kukupigia au kufika katika biashara yako. Suala la ugeni hapa linakuwa halipo maana tayari kunakuwa na kitu kinaitwa (field of experience) hali fulani ya kuzoeana au mteja kuwa na taarifa zaidi kuhusu biashara yako. Hivyo mnaanza kuongea kadiri mnavyoona inafaa ili kuendelea kujenga ukaribu.

Kama kuna namba kubwa ya wateja unaowahitaji kwenye biashara yako ni wateja tarajiwa wengi. Hapa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa ufuatiliaji wa wateja wako.

Mfumo huo unaitwa Customer Relationship Management (CRM). Huu ni mfumo wa kufuatilia wateja wako. Ndani ya mfumo huu unaweka taarifa za wateja wako kama jina la mteja, mawasiliano, maumivu, mahali alipo, kampuni, siku ya kwanza kumfikia, pamoja na taarifa zingine muhimu kuhusu mteja. Uwepo wa taarifa hizi unakusaidia wewe katika kuendelea kumfuatilia zaidi, yaani unapoongea naye uanzie wapi.

Katika kutumia mfumo huu unahitaji kuwa na “sheet” au “excel” ambapo kila unapofanya naye mawasiliano unajaza namna mazungumzo yenu yalivyokuwa. Kama ameweka ahadi unajaza inapofika tarehe ya ahadi husika unamkumbusha. Lengo ni kuendelea kuwa naye karibu.

Uwepo wa wateja tarajiwa ni sawa na kisima cha maji katika nyumba yako. Kisima kinakuwa na mipira inayoelekea katika sehemu tofauti. Siku ukiona mipira haipitishi maji moja kwa moja unajua maji kwenye kisima yameisha. Unafanya utaratibu wa kujaza maji mengine. Sasa kwenye mauzo unatakwa kuhakikisha bomba lako lina jaa muda wote ili wateja wakipungua unaingia kwenye orodha yao na kuanza kuwatafuta wateja tarajiwa wengine.

Mtaja tarajiwa anapofuatiliwa kwa ukaribu bila kumuacha akapoa ndiye huja kuwa mteja kamili. Hapa maana yake anakuwa tayari amejiridhisha kuwa wewe ni mtu sahihi wa kumpatia huduma. Anakuwa hana wasiwasi wowote tofauti na mteja lengwa. Kupitia ufuatiliaji unaofanya ndiyo humfanya afanye maamuzi na kuwa mteja kamili.

Sifa Za Mteja Tarajiwa;

Moja; Mteja tarajiwa anakuwa bado hajatoa pesa yake. Kwa lugha rahisi hajafanya manunuzi yoyote.

Mbili; Kuna kitu anajua kuhusu biashara yako. Iwe ni kupitia usakaji, simu au matangazo mengine.

Njia Za Kupata Wateja Tarajiwa;

Moja; Kuongea na marafiki na kuwatumia jumbe mbalimbali.

Mbili; Kushiriki kwenye semina, mikutano au misiba

Tatu; Njia ya rufaa.

Nne; Matangazo mbalimbali ya redio au mitandao ya kijamii.

Tano; Kutoa mafunzo ya bure kuhusiana na biashara yako.

Hatua za kumgeuza mteja tarajiwa kuwa kamili;

Moja; Kusanya taarifa za walioonyesha uhitaji. Hii ni baada ya kuweka tangazo kwenye kurasa za mitandao au mabango. Hapa wanapiga simu au kufika eneo lako.

Mbili; Wachambue wateja wako tarajiwa kuzingatia uhitaji wa haraka au baadaye.

Tatu; Wafanyie ufuatiliaji wateja tarajiwa kulingana na mahitaji yao

Nne; Kamilisha mauzo.
Kupitia ufuatiliaji unajikuta unawageuza wateja tarajiwa kuwa kamili.

Hivyo, kumbadilisha mteja tarajiwa kuwa kamili unahitaji kutumia ushuhuda kwa kiwango kikubwa. Wateja wanahitaji kuona kuna wenzao wamefanya maamuzi ya kujiunga na biashara. Kitendo cha wewe kumshawishi naye kutoa pesa yake ndipo anakua mteja kamili.

Ipi njia bora unayotumia kutengeneza wateja tarajiwa?

Imeandaliwa na Lackius Robert Mkufunzi Wa Mauzo na Mwandishi.
Mawasiliano 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz

Leave a comment