Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Mambo Muhimu Ya Kujifunza Kabla Hujakutana Na Mteja

Huwa tunakua katika hali ya ugumu fulani pale ambapo tunataka kukutana na mtu ambaye hatumjui. Unakutana na mteja ambaye hamjuani na ugumu unakuja pale ambapo unafikiria je, utaenda kuongea naye nini?

Kama unapata shida na hujui ukikutana na mteja utaongea naye nini, habari njema ni kwamba, kupitia makala hii ya leo, unakwenda kupata suluhisho hilo.

Kabla ya kukutana na mteja wako mara ya kwanza, kitu unachotakiwa kufanya ni kujua zaidi juu ya mteja wako.

Unapaswa kuwa mpelelezi au shushushu kwa mteja wako. Pata taarifa muhimu kutoka kwa mteja wako.
Jua anapenda nini kwa mfano, peleleza anapendelea michezo ya aina gani? Kama ni mpira wa miguu, je yeye ni shabiki wa timu gani? Ukishajua hilo itakusaidia kujifunza kuhusu upande wake na hata mkikutana unakuwa na kitu cha kuzungumza.

Ugumu wa watu wengi unakuja pale ambapo anaenda kukutana na mteja halafu hajui nini ataenda kuongea naye.

Kabla hujakutana na mteja, chunguza kwanza vitu ambavyo mteja wako anapendelea na hata ukikutana naye unaongea naye vitu hivyo.

Ukiwa upande wake, ataona wewe uko kama yeye. Na ataondoa ile hali ya ugeni kwako na atakuchukulia kuwa wewe uko kama yeye na itakua rahisi kuongea.

Ukikutana na mteja anapendelea mpira, na wewe fuatilia kile anachopenda na wewe kuwa upande wa mteja wako.

Tafuta kitu kimoja ambacho kitawaunganisha wewe na mteja wako.
Viko vitu vingi ambavyo watu wanapendelea hivyo ni wajibu wako kujua hilo.

Raisi mmoja wa Marekani kabla ya kukutana na mtu asiyemjua alikuwa anajifunza kwanza kile anachopenda mtu yule atakayekutana naye. Ni rahisi kukubaliana na mtu kama utaonesha uko upande wake.

Hatua ya kuchukua leo; kama unataka kukutana na mteja au mtu yeyote yule ambaye hamjuani, kuwa mpelelezi na jifunze vile anavyopendelea ili ukikutana naye unaongea juu ya vitu hivyo.

Bila kujua kile anachopendelea mteja wako, inakuwa ni rahisi.
Kuwa mpelelezi, peleleza wateja wako taarifa muhimu utakazitumia kumshawishi kununua au kukubali na wewe. Jenga, mahusiano na mteja wako ili uweze kujenga ushawishi na kukubalika.

Kitu kimoja zaidi, pata kitabu chako cha MAUZO NI MAHUSIANO ili kikusaidie kupata mbinu za kujenga mahusiano bora na wateja wako na kuwafanya kuwa wako daima.

Na ukiwafanya wateja wako kuwa kwako daima maana yake mauzo kwako siyo tatizo tena. Narudia tena, kama bado hujasoma kitabu cha MAUZO NI MAHUSIANO, piga hii namba 0717101505 sema uko wapi utatumiwa kitabu chako.
Watu wengi wameshapata nakala zao kama na wewe bado fanya fasta upate yako kabla hazijaisha.

Kutoka kwa rafiki na muuzaji mwenzako,
CIO, Mwl Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa Chuo Cha Mauzo,
Barua pepe; makamu@mauzo.tz
Simu; 0717101505 wasapu na kawaida/0767101504.
http://www.t.me/chuochamauzo
www.mauzo.tz

Leave a comment