Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Ucheleweshaji Na Namna Unavyowaondoa Wateja Katika Biashara Yetu

Ni asubuhi na mapema, umeenda dukani kununua sukari na mkate. Umefika na kumpatia mhudumiaji pesa yako ili akupe bidhaa. Mara baada ya kumpatia pesa, anaanza kuzunguka zunguka. Anatafuta kabati hii mara ile na muda unazidi kusogea, hadi unapewa bidhaa dakika kumi zimekata. Je, utarudi tena kuchukua vitu pale?

Mbili; Umeenda kwenye mgahawa kwa ajili ya kupata chakula cha mchana. Ukafika vizuri na kuagiza chakula. Mhudumiaji akakwambia dakika tatu chakula chako kinakuwa tayari mezani. Akwambia unaweza kunawa mazima ili chakula kikija iwe rahisi kuanza kukishughulikia.

Dakika tano za kwanza zimeisha. Wakati huo unamuona mhudumiaji anaangaika na mambo mengine wala sio kutafuta chakula chako. Dakika kumi huyoo! Unajaribu kumuita, vipi oda yangu mbona siletewi? Anakuuza, hivi uliagiza nini vile?
Je, utakuwa tayari kumjibu ili akusubilishe tena au utaondoka?

Tatu; Umeona bidhaa mtandaoni ukaiagiza. Mhusika akakwambia ndani ya saa 24 inakufikia. Na bidhaa hii ipo karibu na eneo uliopo. Mkaweka miadi safi na ukaanza kusubiri. Saa 24 zikapita. Ukavuta vuta muda. Saa sita zikaongezeka, ukasema labda usafiri. Saa 12 zikakata bila taarifa yoyote.

Umejikatia tamaa baada ya kusubiri sana, unaona mhusika anapiga simu. Je, utaipokea?

Hayo ni machache tunayokutana nayo katika kuwahudumia wateja. Tafiti zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 84% ya huduma huhusisha ucheleweshwaji wa bidhaa kumfikia mteja.

Asilimia hizi ni nyingi. Tunahitaji kuweka juhudi kubwa kuhakikisha wateja wetu hawaoni kero kwetu. Zingatia tips hizi ili kupunguza hali ya mteja kuona anacheleweshwa;

Moja; Kuwa na kitu cha kuwafanya wawe bize nacho.
Mfano ukiingia kwenye gari zinazosafiri masafa marefu, hospital na sehemu zingine huwa wanaweka TV. Sio urembo, bali ni kutaka akili yako isione kama unachelewa bali iweke nguvu katika kuangalia TV huku muda wako wa kuhudumiwa ufikiwe.

Mbili; Timiza ahadi.
Moja ya eneo linaloleta shida katika zama hizi ni kutotimizwa kwa ahadi nyingi. Tunaongea sana kuliko kutenda.

Tatu; Kuwa mkweli.
Mafanikio makuu katika mauzo yapo kwenye ukweli. Hata kama sio asilimia zote lakini kwa kiasi utakusaidia wateja kukuamini.

Nne; Fanyia kazi mrejesho wa wateja.

Tano; Washukuru wateja.
Waambie asante sana kwa kusubiri huduma yetu. Tunaamini uharaka ni kitu muhimu sana tutajitahidi.

Fanyia kazi haya machache uliyojifunza leo ili usiendelee kuwapoteza wateja wako. Weka akilini mauzo bila wateja hayajamakilika. Wape huduma nzuri nafuu na haraka utawabakiza milele.

Kwa hayo na mengine mengi karibu sana katika program zetu za Chuo Cha Mauzo ujifunze namna bora kukuza biashara yako. Tuwasiliane 0767702659, maarifarobert@gmail.com au mkufunzi@mauzo.tz

Imeandaliwa na Lackius Robert Mkufunzi wa mauzo na mwandishi. Tufuatilie pia www.mauzo.tz

Leave a comment