Mpendwa muuzaji,
Hakuna zama ambazo ni rahisi kuuza kama zama hizi tunazoishi sasa. Kama huuzi katika zama hizi na una huduma nzuri au bidhaa basi hiyo ni shida yako binafsi.
Hii ni kama vile unakufa na kiu, wakati uko kisimani.
Kama unasoma hapa, halafu unahangaika huuzi, basi utakua unajipunja sana. Habari njema ni kwamba, ukiwa na zana kuu ya mauzo ambayo ni simu unaweza kuuza sana.
Sina uhakika kama itakufaa lakini ukiwa na simu utaweza kuuza hata huku ukiwa umekaa nyumbani.
Kama huna wateja, huuzi umekaa kwenye eneo la biashara na unalalamika hujauza, iko sehemu ya kuanzia.
Sehemu pekee ya kuanzia kama mauzo yako ni duni au huna wateja ni kwenye simu yako.
Simu yako ina majina ya watu wengi sana. Je, majina ya watu hao wanafahamu juu ya kile unachouza au huduma unayotoa?
Huuzi, je, umechukua hatua ya kuwapigia simu wateja wako ili kuwaomba wakupatie oda?
Umepiga simu kuwasalimia wateja wako na kujua wanaendeleaje?
Mauzo ni mahusiano. Lazima uhusiane na wateja wako ili uweze kuuza.
Kama huuzi, huna wateja anzia kwenye simu yako. Wapigie simu wale ambao wako kwenye simu yako na kuwaeleza juu ya kile unachouza.
Kwa mfano, wapigie simu wateja tarajiwa ambao wako kwenye simu yako, wasalimie, waambie, je, una fahamu kwamba tunauza moja mbili tatu?
Hapo hapo, unamuomba akusaidie kupata wateja wapya wengine wa rufaa.
Vitabu vya dini vinasema, ombeni nanyi mtapewa. Piga siku kwa wateja wako na omba oda. Waambie kile ambacho wewe unauza au huduma unayotoa.
Maisha ni mauzo. Kama huuzi, basi jua unauziwa. Kila mmoja wetu kuna kitu ambacho anauza ndiyo maana anapata fedha kwa ajili ya kuendesha maisha yake.
Bila mauzo, hakuna maisha. Ni katika mauzo ndiyo tunapata ushindi wa kweli.
Usianze kusema, ooh sasa nikiwapigia simu watanionaje? Wewe fanya kazi yako, waambie wajue na kama wakijua siku wakiwa na uhitaji watakutafutia wateja au hata wao wenyewe watakuja kununua kwako.
Kama unakaa siku nzima uko kwenye biashara na huuzi, basi ni ishara ya kutotumia vizuri simu yako. Tumia simu vizuri sana ili kupata wateja wapya na hata wa zamani ili uendelee kuwahudumia.
Hatua ya kuchukua leo; piga kelele kwa ajili ya mauzo yako. Piga kelele kwa kutumia simu yako.
Waambie watu unauza nini na wajue hilo. Ni bora kufanya wakajua hata wasiponunua kuliko kutokufanya.
Kazi yako wewe ni kufanya, matokeo yako nje ya uwezo wako.
Wapigie simu wateja wako, anzia kwenye simu yako. Wapigie simu watu ambao umehifadhi namba zao kwenye simu yako. Waambie wewe unauza bidhaa au huduma fulani aje kununua au akutafutie watu kuja kununua.
Usikae dukani huna wateja na ukaridhika kama hujawapigia simu wateja wako. Ongeza mauzo zaidi kwa kutumia simu yako. Tumia simu kupigia simu wateja wako wote na kuwaambia habari njema kuhusu kile ambacho wewe unauza.
Ukiona una shida kwenye biashara yako, anzia kwenye simu yako. Simu yako ni suluhisho namba moja la mauzo kwenye biashara yako.
Hiki ni kionjo tu kutoka kwenye kitabu cha MAUZO NI MAHUSIANO. Ninakusihi uweke oda yako mapema, kwani watakaoweka oda yao mapema watapata punguzo. Kaa Kwenye orodha mapema ili upate zawadi pamoja na kitabu chako.
Ukijenga mahusiano na mteja wako, unatakiwa kuyaimarisha. Kwa sababu MAUZO NI MAHUSIANO, hauuzi mara moja, bali unamwitaji mteja uliyempata maisha yako yote ili aendelee kununua.
Mwisho, mauzo ni njia sahihi ya kuweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako. Mauzo ndiyo ushindi wa uhakika, ukipata umepata, hivyo usipange kukosa kusoma kitabu hiko, siyo tu kitakusaidia sana kwenye mauzo, bali pia kuboresha mahusiano yako, utakuja kunishukuru baadaye baada ya kukisoma kitabu hiko.
Naomba unisaidie kitu kidogo, naomba unisaidie kuisambaza makala hii kwa mtu wako mmoja tu unayempenda ambaye unataka naye aje kunufaika kama utakavyonufaika wewe na kitabu cha MAUZO NI MAHUSIANO.
Hatua ya kuchukua leo; weka oda yako sasa hivi kwenda namba 0717101505 ili ujihakikishie nafasi ya kupata kitabu kwani watu wengi wameweka oda.
Kutoka kwa rafiki na muuzaji mwenzako,
CIO, Mwl Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa Chuo Cha Mauzo,
Barua pepe; makamu@mauzo.tz
Simu; 0717101505 wasapu na kawaida/0767101504.
http://www.t.me/chuochamauzo
www.mauzo.tz