Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Nguvu Ya Simu Na Namna Inavyoleta Ushindi Katika Mauzo

Kitu kigumu na kinachoogopesha watu ni kuongea mbele za watu. Kwa kuwa ni kigumu basi njia rahisi ya kufanyia kazi ni kupiga simu. Hii ni njia inayotumika mara nyingi kuwasiliana na wateja. Maana sio kila mteja unaweza kumtembelea.

Mambo ya kuzingatia wakati wa kupiga simu;

Moja; Maandalizi.
Hapa unajiandaa kiakili kwa ajili ya kupiga simu.

Mbili; Shauku.
Shauku inaendaana na sauti kuwa juu. Sauti yako ina nguvu ya ushawishi. Hapa anza na urafiki, usianze kama mtu unayetaka kuuza. Pia sauti yako iwe inasikika vema kabisa.

Tatu; Skripti ya mauzo.
Hii ndio inakuongoza wakati wa mazungumzo. Usipige bila kuwa na mpangilio wowote. Kuanzia kujitambulisha hadi mwisho. Script izingatie.
(I) Umakini wa mteja
(II) Maslahi Ya Mteja
(III) Tamaa
(IV) Hatua

Ili kukumbuka script ya mauzo tumia(AIDA) ikiwa na maana Attention, Interest, Desire na Action. Na hivi ndivyo nilivyoelezea hapo juu.

Nne; Kusikiliza.
Wauzaji ni waongeaji na hili linathiri sana mauzo. Unapokuwa unaongea sana bila kumpatia nafasi msikilizaji kuongea inafanya ukose umakini na kumuelewa vizuri. Ili uuze zaidi unatakiwa kuwa msikilizaji badala ya kuwa muongeaji.

Mungu amekupa masikio mawili na mdomo mmoja. Mdomo mmoja maana yake unaongea kidogo, masikio mawili unasikiliza zaidi.
Kwa bahati mbaya wauzaji wengi tumekuwa tunaongea sana mpaka tunaboa wateja wetu.

Tafiti zinaonyesha wauzaji hutumia asilimia 80 hadi 90% ya mazungumzo wakati wa mauzo. Kitu kinachowafanya wengi kushindwa kuuza zaidi. Unachotakiwa kufanya wewe ni kuwa msikilizaji wakati wa mazungumzo.

Tano; Mhusika.
Hapa unapaswa kujua ni mhusika yupi unaongea naye ili uende kwenye mada kuu.

Sita; Usimpinge mteja.
Wakati unazungumza na mtu kwa njia ya simu ikiwa kiongea kitu kisicho sahihi, usimpinge wewe msikilize tu kisha endelea na mzungumzo yenu.

Madhumuni ya kupiga simu;
Moja; Kuomba miadi
Mbili; Kufuatilia na mengine kulingana na mapokeo yake

Simu Ya Ushindi

Wauzaji wengi wanashindwa kuuza na kukuza biashara zao kwa sababu wanakosa kupangilia mazungumzo yao. Ili kuwa na uwezo wa kutengeneza mahusiano mazuri na kuongoza mawasiliano, lazima uwe na mpangilio mzuri wa nini kinaenda kufuata. Iwe ni mkutano wa pamoja au njia ya simu na hapa chini nimekuwekea hatua za kuzingatia;

Moja; Ruhusu mazungumzo na mtambue mteja hii itafanya upate nafasi ya kumsikiliza na kile kinachomsibu.

Mbili; Shirikisha ajenda.
Kuwa na kitu mnachoenda kuzungumzia. Usianze kumuomba akwambie kitu. Wewe shirikisha kitu kisha mkiongelee. Epuka kumwambia mteja, “niambie “. Hii inaboa sana.

Tatu; Muondoe wasiwasi.
Ikiwa kuna kitu kinamsumbua mwambie matokeo unayoenda kumpatia. Gusia suala lake kwa muda mchache tu. Hapa mpe sababu ya kumfanya aendelee kukupa nafasi kugusia namna biashara yako inavyoenda kumsaidia kupata anachotaka.

Tano; Uliza maswali.
Yanaweza kuwa binafsi, kimtego au kibiashara.

Sita; Jibu mapingamizi.
Iikiwa pingamizi limejitokeza lijibu.

Saba; Uza, baada ya yeye kuona manufaa muuzie bidhaa.

Nane; Panga mkutano au mazungumzo mengine. Kama hajaweza kununua.

Njia ya simu ikitumika vizuri inaenda kuleta mchango mkubwa katika kuikuza biashara yako. Unachotakiwa ni kuanza taratibu kupiga simu. Kadiri muda utakavyoenda ndivyo utagundua unapata uzoefu zaidi. Kikubwa zingatia ujasiri. Jiamini katika maongezi yako utauza zaidi.

Kazi yako kuu ni kujiandaa vema na kuwapigia wateja wako. Kwa hayo na mengine mengi karibu kwenye programu zetu za Chuo Cha Mauzo Tanzania. Huku Unajifunza hatua hatua jinsi ya kuongeza mauzo angalau mara mbili kwa mwaka. Pia, kuna vitabu vya mauzo vinavyoenda kukupa maarifa sahihi.

Imeandaliwa na Lackius Robert Mkufunzi, Mjasiriamali na Mwandishi tuwasiliane 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz

Karibu tujifunze zaidi.

Leave a comment