Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Mbinu Tatu Za Ukamilishaji Wa Mauzo 10-12

Ukamilishaji ni hatua muhimu kwa kila mtu kupata kila anachotaka kwenye maisha yake. Pale tu mteja anapoonesha nia ya kununua, kamilisha mauzo haraka.
Usiogope, usione haya au aibu kumwambia lipia.

Ni wajibu wako wa kimaadili kuuza. Hakuna ustaarabu mwingine zaidi ya kuuza, acha kuonekana wewe ni mtakatifu wa kijamii kwamba ukiwaambia watu lipie utaonekana una tamaa, acha uonekane una tamaa lakini unaingiza fedha.
Kutaka kuonekana ni mtakuwa na kuogopa watu watakuchukuliaje hakutakusaidia wewe kuingiza fedha kwenye biashara.

Hakuna gharama kubwa kwenye maisha kama mtu kushindwa kukamilisha mauzo au ushawishi kwenye ndoto na mawazo aliyonayo. Kushindwa kukamilisha kumekuwa kunawachosha watu na kuwafanya washindwe kujiamini. Wale wanaoshindwa kukamilisha huwa wanakata tamaa na kukubali kushindwa.

Kwa hili tunaweza kusema uwezo wa kukamilisha ndiyo hitaji la kwanza kwa mtu kufanikiwa kwenye maisha. Kwa sababu ndiyo njia ya mtu kuweza kushawishi na kupata uungwaji mkono na watu muhimu kwenye kile anachofanya. Biashara zinashindwa kwa sababu hazipati mapato ya kutosha kutokana na kutokukamilisha mauzo.

Watu huweza kutoa sababu mbalimbali kwa nini biashara zinashindwa, lakini ya kwanza kabisa ni hiyo ya kushindwa kukamilisha mauzo na hata mipango mingine inayokuwepo.

Leo tunakwenda kujifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo na mbinu hizo ni;

Ukamilishaji wa kuongea na mwenza – 4.

Mteja anakuambia anahitaji kuongea na mwenza wake kwanza.

Wewe mjibu hivi mteja,
“Nakuelewa na kama wewe na mwenza wako huwa mnaongea kama mimi ninavyoongea na mwenza wangu, basi anajua uko hapa na unachofanya.

Hivyo tukamilishe hili kama hakuna kikwazo kingine. Weka sahihi yako hapa au lipia sasa ili uende ukaifurahie bidhaa au huduma yako.

” Ufafanuzi; ukamilishaji huu unatumia kudhania kwamba wanaelewana vizuri na hivyo kwenda moja kwa moja kwenye ukamilishaji badala ya kupoteza muda.

Ukamilishaji wa upande usiokuwepo – 1.

Hapa mteja anakupa pingamizi la aongee kwanza na mtu mwingine. Pale mteja anapokuambia hivyo, mwambie hivi,
“Tukubaliane kwenye bei, halafu kuletewa itasubiri mwenza wako akubali. Je hiyo iko sawa?

Akijibu sawa, tayari ameshakubaliana na kile unachouza hivyo Mwambe kinachofuata baada ya hapa ni wewe kukamilisha malipo ili uondoke na bidhaa au huduma yako.
Kwa mfano, kinachofuata baada ya hapa ni wewe kukamilisha malipo ili uende ukakifurahie kitabu chako cha CHUO CHA MAUZO.

” Ufafanuzi; ukamilishaji huu unapaswa kutumika kama hatua ya mwisho pale mtu anaposisitiza lazima kwanza aongee na kukubaliana na mwingine. Usitumie hii kupitiliza.

Ukamilishaji wa upande usiokuwepo – 2.

Unamuuliza mteja,
“Je mwenza wako anakubaliana na hali uliyonayo sasa na jinsi inavyokugharimu? Kama hakuna kitakachobadilika, zaidi ya hali yako kuwa bora zaidi, kwa hakika atakubaliana na mabadiliko hayo.

” Ufafanuzi; ukamilishaji huu ni sawa na uliopita, ila unapima uhalali wa pingamizi analokuwa anatoa mtu. Wengi wanashindwa kukamilisha mauzo kwa kusubiri mtu akaongee na mwenza wake wakati siyo lazima afanye hivyo.

Hatua ya kuchukua leo; nenda kazifanyie kazi hizi mbinu na utakuja kutushukuru baadaye kwa namna utakavyonufaika na mbinu hizi.

Mwl.Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz

Leave a comment