Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Mauzo Ya Ziada Na Namma Yanavyokuza Biashara Yako

Mauzo ya ziada, ni mauzo yanayofanyika baada ya mauzo makuu kukamilika. Au ni lile wazo jipya unalomuingizia mteja wakati wa kukamilisha mauzo. Mfano, kama unauza spea za magari au pikipiki mteja akanunua oil. Unapaswa kumshawishi akanunua oil filter. Hapo umefanya mauzo ya ziada.

Kwahiyo hapo mauzo ya ziada ni oil filter. Mfano mwingine, mteja amenunua simu. Akafanya malipo, baada ya hapo ukamshawishi kununua “protector”, “cover” au “earphone”. Mteja akikubali, hapo umefanya mauzo ya ziada.

Wakati mwingine mauzo ya ziada yanaweza kufanyika kabla ya mauzo makuu. Mteja anaweza kuja anahitaji bidhaa ugali dagaa, ambao bei ni ndogo tofauti na pilau nyama. Hapo pia, umefanya mauzo ya ziada. Au mteja anataka simu ya itel, ukamshawishi kununua I phone. Hapo umefanya mauzo ya ziada.

Mambo ya kuzingatia ili kuuza mauzo ya ziada;
Moja; Mjue mteja wako.
Hapa jua mipango yake, mahitaji au malengo. Hii itakusaidia kumpendekezea bidhaa inayokidhi matakwa yake.

Mbili; Ijue biashara yako.
Malengo makubwa ni kuhakikisha unajua bidhaa ipi inaendana na bidhaa fulani. Ili wakati wa mazungumzo umshawishi mteja.

Tatu; Msikilize mteja.
Wauzaji wanasifika kuongea sana. Wewe usifanye hivyo, msikilize Kisha msaidie hitaji lake.

Wakati upi kufanya mauzo ya ziada?
Mara baada ya mauzo makuu kukamilika na pesa ukawa nayo mkononi. Wakati mwingine inategemea na maumivu ya mteja.

Note; Kwenye kufanya mauzo ya ziada epuka kumdhania mteja kuwa hana pesa ya kutosha , amelalamika sana. Timiza wajibu wako. Acha yeye mwenyewe akwambie hapana.

Pesa haijionyeshi usoni mwa mtu. Ni wewe kuwa makini na kumpatia maelezo mazuri yenye ushawishi kwa kina.

Hitimisho. Kila mteja anayekuja kwako usiache kufanya mauzo ya ziada. Huo ni wajibu wako wa kimaadili kuufanya.

Je, unafanya mauzo ya ziada? Wakati ndio huu kukuza mauzo yako kupitia mauzo ya ziada.

Imeandaliwa na Lackius Robert Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo na Mwandishi. Wasiliana naye 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz

Leave a comment