Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Ngazi Za Kupandisha Wateja; (1)Mteja Lengwa.

Mteja lengwa, huyu ni mteja ambaye biashara yako au huduma inamlenga. Kwa kingereza anaitwa “suspect”, ikiwa na maana ya mtuhumiwa. Kama tunavyojua mtuhumiwa ni mtu anayeshukiwa kutenda uhalifu ambao haujathibitishwa.

Mteja hapa sio kwamba ni mtuhumiwa. Bali neno hili kwenye mauzo linatumika katika mazingira ya kuonyesha unamdhania, lakini unakuwa huna uhakika kama anaweza kumudu gharama za huduma yako au kuhitaji bidhaa kwa muda huo.

Jinsi Ya Kupata Wateja Lengwa;
Moja; Matangazo.
Kupitia njia mbalimbali kama Redio, “sponsored ads” kwenye mitandao ya kijamii, Status, tovuti, banner, fly na njia zingine za urushaji wa matangazo.

Mbili; Usakaji.
Hapa unawatembelea wauzaji tofauti tofauti huku ukiwaelezea kuhusu bidhaa yako. Hivyo, na wao wanajua uwepo wa biashara yako.

Tatu; Simu.
Hapa unapiga simu mpya outbound kwa wateja lengwa. Madhumuni makubwa ni kuwafahamisha uwepo wako sokoni na biashara kwa ujumla.

Mfano; kama unauza spea za magari au pikipiki, unapokutana na mtu mwenye duka la kuuza spea au mtu anayetengeneza magari, huyo moja kwa moja ni mteja wako lengwa. Muda wowote anaweza kuhitaji bidhaa yako.

Nne; Rufaa.
Mara baada ya kumuuzia mteja akafurahia huduma yako, unamuomba mtu mmoja anayemdania anaweza kunufaika na bidhaa yako kama yeye. Anapokupatia mteja unampigia kumshirikisha kuhusu biashara yako. Maana yake anajua uwepo wao na pia wanajua uwepo wako..

Njia ya rufaa ni njia nzuri kwako kupata wateja muhimu wa kushughulika nao. Kwa sababu mteja anayenunua kwako anakupatia mtu anayemdhania. Baada ya hapo unaanza kumfanyia kazi. Hivyo ili uendelee kupata wateja wapya unahitaji kuomba rufaa kwa wateja ulionao.

Tafuta namna ya kuwachambua wateja wako. Hapa unaweza kuwa na daftari unayoandika watu unaotaka kushughulika nao au wateja wako. Baada ya hapo unaona namna gani mnaweza kufanya biashara kubwa.

Hii inakusaidia kuwa na mahali pa kuanzia au kuangalia linapofika suala la kutafuta wateja muhimu. Kuwa na wateja wa ndoto yako. Hii ni muhimu sana pale unapokuwa unaandaa idadi ya wateja unaotaka kushughulika nao. Maana ukiwa nao inakuwa rahisi kuwa unawafuatilia kwa ukaribu mkubwa bila kuchoka. Cha kuzingatia hapa idadi ya wateja wako wa ndoto inapaswa kuwa kubwa ili usije kukosa mauzo panapotokea changamoto.

Walenge Wenye Mamlaka Ya Juuu.

Kitu kingine unachopaswa kuzingatia ni kuwalenga wafanya maamuzi au watu walio vitengo vya juu kwenye kampuni mbalimbali. Ukiwalenga watu wa chini kuuza litakuwa ni suala gumu tofauti na ukiwalenga walio katika nafasi za juu kwenye makapuni makubwa. Kwa kuwa hofu inatutawala wengi wetu ndiyo maana tunaishia katika kupata watu walio katika nafasi za kawaida.

Lakini kama umedhamiria kuiendeleza na kuikuza biashara yako basi jua kushulika na watu wa vitengo vya juu itakusaidia sana.
Kuchagua wateja lengwa ni hatua ya kwanza kubwa kwenye kukuza mauzo.

Unapokuwa nayo inakuwa kama silaha yako unacheza nayo hadi unafanikiwa kuuza zaidi. Maana mteja lengwa unapokuwa umemfikia ukamshirikisha kuhusu biashara au huduma yako tayari anabadilika kutoka mteja lengwa kuwa mteja tarajiwa aliyetengenezwa.

Mteja anakuwa lengwa kabla ya kumfikia, yaani akiwa katika fikra zako. Lakini kitendo cha kumfikia akajua wewe ni nani kwenye huduma yako, huyo tayari sio tena mteja lengwa. Maana sifa pekee ya mteja lengwa anakuwa hakujui kama upo kwenye dunia hii. Maisha yake yanaendelea vizuri, anaweza kuendelea kuumizwa na bei, huduma mbaya. Bila kujua kama kuna mahali anaweza kupata huduma nzuri.

Kwa hiyo, unapokuwa umemfikia anakuwa mteja tarajiwa. Unaanza kumweka kwenye matarajio kwamba siku moja atakuja kuungana na huduma au biashara yako.

Mambo ya kujiuliza na kuzingatia wakati wa kutafuta wateja muhimu;
Wateja wangu ni wapi?
Wanapatikana wapi na mawasiliano yao?
Kwanini ninawalenga?
Je, wananua wapi?

Fanyia kazi yote uliyojifunza katika makala hii ili uwe na wateja wengi tarajiwa kama tutakavyojifunza masomo yanayofuata.

Imeandaliwa na Lackius Robert Mkufunzi Wa Mauzo na Mwandishi. Tuwasiliane 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz

Leave a comment