Mpendwa muuzaji bora kuwahi kutokea,
Kila mmoja wetu anapenda kupata wateja wazuri na wanaoaminika. Kazi yako kubwa kama muuzaji ni kujenga wateja wanaoaminika kwenye biashara.
Ili uweze kupata wateja wanaoaminika kwenye biashara yako, unapaswa kwanza wewe jenga kujenga kuaminika kwa wateja wako.
Huwezi kujenga wateja wanaoaminika kama wewe mwenyewe hujaaminika.
Jenga kuaminika, wafanye watu wakutegemee kwa kitu fulani. Waahidi watu kisha tekeleza kama ulivyoahidi.
Kadiri watu wanavyokuamini, ndivyo wanavyojenga imani na wewe.
Watu wanavyokuwa na imani na wewe wanajenga uhakika. Na kumbuka, uaminifu unajengwa mahali penye uhakika. Kuwa mtu wa uhakika na watu watakuamini bila shaka yoyote ile.
Zoezi la kujenga wateja wanaoaminika linaanza na sisi kujenga uaminifu kwa wateja ambao tunajihusisha nao ili nao waweze kujenga mahusiano na sisi.
Hakikisha unajihusisha na watu wanaoaminika. Anza kuaminika na kisha jenga wateja ambao ni waaminifu. Wateja ambao hawaaminiki kwenye biashara yako, watakusumbua.
Unapojenga wateja, hakikisha unajenga wateja wanaoaminika. Na wateja wanaoaminika wanaanza na wewe kuaminika kwanza. Toa huduma bora na thamani kubwa kiasi kwamba wateja wanakuamini.
Mauzo ni mahusiano, hivyo unapohusiana na watu hakikisha, unahusiana na watu waaminifu. Unapojenga mahusiano na wateja wako, hakikisha unajenga mahusiano na wateja wanaoaminika tu. Na wateja ambao hawaaminiki, usijihusishe nao watakusumbua.
Mpendwa muuzaji bora kuwahi kutokea, hivi karibuni kitabu cha MAUZO NI MAHUSIANO kitakusaidia hewani. Endelea kukaa kwenye mkao wa kula, endelea kujiandikisha na kuweka oda. Na niwapongeze wale ambao tayari wameshaweka oda zao na kitabu kinapotoka basi wanakuwa wa kwanza kupata kitabu hicho. Lakini pia, watu wanaoweka oda mapema watapata zawadi, usipange kukosa kusoma kitabu chako cha MAUZO NI MAHUSIANO, utakuja kunishukuru baadaye.
Mwisho, mauzo ni njia sahihi ya kuweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako. Mauzo ndiyo ushindi wa uhakika, ukipata umepata, hivyo usipange kukosa kusoma kitabu hiko, siyo tu kitakusaidia sana kwenye mauzo, bali pia kuboresha mahusiano yako, utakuja kunishukuru baadaye baada ya kukisoma kitabu hiko.
Naomba unisaidie kitu kidogo, naomba unisaidie kuisambaza makala hii kwa mtu wako mmoja tu unayempenda ambaye unataka naye aje kunufaika kama utakavyonufaika wewe na kitabu cha MAUZO NI MAHUSIANO.
Kutoka kwa rafiki na muuzaji mwenzako,
CIO, Mwl Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa Chuo Cha Mauzo,
Barua pepe; makamu@mauzo.tz
Simu; 0717101505 wasapu na kawaida/0767101504.
http://www.t.me/chuochamauzo
www.mauzo.tz