Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Jinsi Neno Kwa Sababu Linavyoweza Kukuongezea Ushawishi Na Mauzo

Rafiki yangu Muuzaji bora kuwahi kutokea,
Kumbuka, HUPATI UNACHOSTAHILI BALI UNACHOSHAWISHI.

Hakuna kitu ambacho tunaweza kukipata kirahisi kwenye maisha yetu bila kuweza kuwashawishi wengine waweze kukubaliana na sisi.

Ukiona wewe umeweza kupata kitu kwenye maisha yako, maana yake umeweza kuwashawishi wengine WAKUBALIANE na wewe na huo ndiyo tunauita ushawishi.

Ziko njia za mkatao ambazo zinamsukuma binadamu kufanya maamuzi haraka bila hata ya kufikiria sana.
Na kwenye ushawishi wa kufanya hivyo, tumia neno kwa sababu.

Neno kwa sababu, ni neno ambalo ukilitumia pale unapoongea na mteja, linamfanya mteja awe na uhakika na kumshawishi kukubaliana na wewe kirahisi.

Kwa mfano, zilishawahi kufanyika tafiti za kuthibitisha hili.
Mtu mmoja alienda kuomba msaada moja kwa kutumia neno kwa sababu na bila kwa sababu.

Kwenye mazingira ya kwanza, alienda kwenye foleni na kuwakuta watu akawaambia naomba niwe wa kwanza kutoa nakala watu wachache walimkubalia.

Akaenda tena katika mazingira ya pili na kutumia neno kwa sababu, alienda akawaambia waliokaa kwenye foloni, naomba niwe wa kwanza kutoa nakala kwa sababu nataka kutoa nakala nyingi alisimia 94 ya watu walikubaliana naye.

Unapokuwa katika mazingira ya kumshawishi mtu, akubaliane na wewe, tumia neno kwa sababu.

Kwa mfano, wewe kama muuzaji, mwambie mteja sina uhakika kama itakufaa lakini chukua bidhaa hii kwa sababu watu wengi ndiyo wanaipenda. Atakua rahisi kukubaliana na wewe kwa sababu umeshaweka neno kwa sababu.

Lakini, ukimwambia mtu bila neno kwa sababu anakuwa hana uhakika sana na kile unachomwambia. Ili kumuondolea mteja WASIWASI, tumia neno kwa sababu.

Neno kwa sababu, linamfanya mtu akose sababu ya kukatalia kwa sababu tayari umeshasema sababu hivyo anaona hana haja ya kukupinga bali ni kukubaliana na wewe tu kirahisi.

Washawishi watu kwa kutumia neno kwa sababu pale unapotaka wakubaliane na wewe. Tumia neno hili kwa sababu kwa nia njema kwa sababu, neno hili lina nguvu ukilitumia vibaya unaweza kuwalaghai watu.

Hatua ya kuchukua leo; kwenye mauzo unayofanya, tumia neno KWA SABABU kuwashawishi watu kwenye kile unachouza utajenga nafasi ya kukubaliwa.

Siyo tu kwenye mauzo ya biashara, bali kila eneo la maisha yako, unapotaka kuwashawishi watu wakubaliane na wewe tumia neno kwa sababu kwani linawafanya watu waliamini kiasi cha kuwa na uhakika kwenye kile unachowambia.

Watu wanataka uhakika na neno kwa sababu linawapa uhakika hivyo wanajikuta wanafanya maamuzi bila hata ya kufikiria sana.

Kauli mbiu yetu ni ; HUPATI UNACHOSTAHILI BALI UNACHOSHAWISHI.

Muuzaji mwenzako,
Mwl Deogratius Kessy
Mawasiliano 0717101505

1 Comment

 • Miraji abdallah
  Posted November 11, 2023 at 10:36 am

  Kwa asili watu wanapenda Sana uhakika na neno kwa sababu linawapa uhakika. Hivyo wanajikuta wanafanya maamuzi bila hata kufikiri Sana.
  Mimi kuanzia Sasa nitajitahidi kujisukuma kutumia neno kwa sababu
  Katika kila ninapokuwa katika mazungumzo ya mauzo ili iwe lahisi kushawishi na kupelekea mteja kukubaliana na kile ninamshauli afanye/ anunue
  Asante mwl DEO

Leave a comment