Mvushe Mteja Kwenye Mapingamizi Ili Umshawishi Kununua
Mapingamizi katika mauzo ni hoja anazoibua mteja kama kikwazo katika mchakato mzima mauzo. Mapingamizi makuuu katika ukamilishaji wa mauzo ni pingamizi la bei, ubora wa bidhaa, muda na mengine mengi.
Inapotokea mteja akaleta mapingamizi badala ya kumwambia umekosea, hapana au kumkatalia. Kitu cha kwanza, unahitaji kukubaliana na pingamizi lake.
Mfano, mteja akisema bei ni kubwa. Unasema; ni kweli bei ni kubwa, lakini kulingana na ubora, unafuu, juhudi au thamani unayoenda kupata ndivyo vinafanya bei kuongezeka.
Wakati mwingine unaanza kumuuzia maswali kama;
Umenunua mara ya mwisho lini?
Unajua nini kuhusu bidhaa hii?
Wewe ulikuwa na kiasi gani?
Kama nikikuuzia kwa bei ya washindani utakuwa tayari kununua?
Kama nikikupunguzia utakuwa tayari kulipia?
Unachopaswa kujua ni kwamba pingamizi katika biashara ni suala la kawaida. Na inapotokea mteja umempa bei na akalipia hapo hapo lazima uwaze sana maswali kama;
Hivi sijapigwa kweli?
Mhh! Au kuna mahali nimekosea?
Ukweli ni kuwa wauzaji wengi tumezoa hali ya kukutana na pingamizi katika mchakato mzima wa mauzo.
Mteja mwenye mapingamizi ni mteja mzuri sana kununua. Maana unatumia mapingamizi yake kununua. Weka akilini ukijibu pingamizi moja utaongeza pingamizi jingine.
Kitu muhimu kujua ni maumivu ya mteja ili umpatie matokeo anayohitaji. Kuna watakaokubali kununua na kuna wateja watakaoendelea kukupa mapingamizi.
Ukimwambia unaenda kuongeza mauzo mara mbili, atakwambia mbona nimekaa kwenye biashara miaka mitano hicho sijawahi kukiona.
Ukimamia bei ni rafiki atakwambia ni kubwa hawezi kuimudu. Ukimwambia ubora atasema muongo na mengine mengi.
Unachopaswa kujua ni kamba mara zote, “wateja wanawapinga sana mauzaji”. Hili ni suala unalopaswa kujua na imepelekea wengi wasiolijua kupoteza biashara zao. Na baadhi wamewachukia baadhi ya wateja bila kujua kuwa kuna namna wanawachukulia kama nilivyoainisha chini;
Wanajua wauzaji ni waongo, waongeaji, wabinafsi na mengine mengi. Ila ukweli ni kuwa wauzaji ni watu wazuri wenye lengo la kuleta suluhu kupitia huduma au biashara zao.
Jinsi ya kukabiliana na mapingamizi ya wateja;
Moja; Kuwa na uelewa wa unachouza. Hii itakusaidia kumpa maelezo ya kutosha kadiri ya maswali yake.
Mbili; Kuwa na “summary ” ya mazungumzo ya mteja. Utafanikiwa ili kwa kuwa mkimya na msikilizaji. Anapoleta pingamizi mrudishe kwenye mazungumzo ya awali. Mwambie lakini mwanzo ulisema unataka bidhaa hii na mengine mengi. Hii inasaidia mteja kuona namna gani umempa nafasi ya kujielezea zaidi.
Tatu; Uliza maswali hasa yale yanayomfanya ajielezee zaidi.
Nne; Vaa uhusika.
Mapingamizi ni jambo la asili katika mauzo. Kwani limekuwepo enzi na enzi. Sio kitu kigeni kwetu. Unapovaa uhusika humuoni mteja kama msumbufu, bali unamuona kama mtu anayehitaji kupata kile anachotaka.
Tano; Ruhusu mteja atoe ya moyoni. Usimkatishe mteja wakati wa mazungumzo. Muache afunguke, huku wewe ukiwa mkimya na msikilizaji. Akiongea ya moyoni anashusha siraha chini na wewe unaanza kumshambulia kwa kumshawishi.
Sita; Mwangalie mteja usoni.
Ikiwa mteja anayekupa pingamizi yupo dukani. Wakati wa mazungumzo usiangaike na vitu vingine. Mpe muda mchache wa kuongea naye huku ukiangalia usoni. Ataona kweli upo kwa ajili ya kumsikiliza na kumsaidia.
Mwisho kabisa chagua maneno mazuri ya kuongea kwa mteja itakusaidia sana katika uwasilishaji wako, na kukabili mapingamizi hayo.
Njia rahisi ninayokupa ni hii, vikwazo havitakuwa mwisho wako. Unachopaswa ni kujua kuwa vipingamizi vipo kwenye maeneo mbalimbali ya maisha.
Endelea kuweka akilini kuwa; mauzo ndiyo kitu cha muhimu na msingi katika biashara. Bila mauzo hakuna kinachofanyika. Ni wewe kukaa kwenye mchakato sahihi na kuuza licha ya vikwazo.
Wakati mwingine unaweza kuwa unahitaji kumuona bosi fulani katika kampuni fulani lakini unakutana na mapingamizi madogo madogo kwa watu wa chini wakiwemo walinzi na watu wa mapokezi.
Kila unapofika unaambiwa mara bosi amesafiri, mara yupo kwenye mkutano sababu zinakuwa haziishi. Ni wewe kufungua moyo na kukubali hali unayokutana nayo kisha kuikabili.
Je, ni vitu gani unafanya kumvusha mteja kwenye mapingamizi?
Karibu utoe maoni yako hapa hapa.
Habari njema ni kwamba Chuo Cha Mauzo Tanzania tunazo program tofauti za mafunzo ya namna ya kukabiliana na wateja. Pia, tunavyo vitabu kama Chuo Cha Mauzo, MAUZO NI HUDUMA, RAHA, MAHUSIANO. Madhumuni makubwa ni kukupa maarifa sahihi. Lengo ni kukusaidia kuikuza biashara yako angalau mara mbili kwa mwaka tuwasiliane 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz
Imeandaliwa na Mkufunzi Lackius Robert, Mwandishi na Mjasiriamali.
Karibu tujifunze zaidi.
1 Comment
Faraji
Chagua maneno mazuri ya kusema wkt unazungumza na mteja