Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Ufuatiliaji Wenye Tija Unaoenda Kuongeza Mauzo Yako

Ndugu, Ufuatiliaji ni kitendo cha kuhakikisha kila shughuli inapaswa kuwa kama ilivyokusudiwa. Lengo kuongeza ufanisi wa kampuni au biashara au shughuli yeyote.

Katika ulimwengu wa biashara ni biashara chache unazokamilika siku ya kwanza na mteja. Yaani mteja analipia pesa. Lakini tafiti zinaonyesha asilimia 80% ya mauzo yanahitaji ufanye ufuatiliaji sio chini ya mara 5 kuzikamilisha.

Usipofuatilia utafanana na katoto kasikotembea, kanasema mama anapika chakula kizuri. Hii ni kwa sababu kapo nyumbani kanasubiri mama alete chakula.

Ndivyo ilivyo kwa wateja. Utaendelea kubakia hapo bila kukukua. Maana unategemea wateja wajilete wenyewe katika biashara yako.

Kwanini tunafanya ufuatiliaji?

Ni kwa sababu tunahitaji kuwa karibu na wateja wetu. Tunahitaji wajue mawili matatu kuhusu huduma zetu.

Mteja anawindwa na wauzaji wengi. Namna pekee ya kumfanya awe angalau karibu yetu ni kupitia kumfuatilia.

Baadhi ya njia unazoweza kutumia kuwafuatilia wateja ni kupiga simu, kuwatembelea, kuwapa zawadi, kuwatamkia siku njema katika kumbukizi za kuzaliwa kwao. Sherehe, sikukuu na matukio na zingine nyingi.

Zoezi la Ufuatiliaji linapaswa kufanywa mara kwa mara angalau kila wiki uguse wateja wengi kama sio wote.

Umuhimu wa kufanya ufuatiliaji;
Moja; Inajenga mahusiano mazuri.
Mbili; Inajenga uaminifu.
Tatu; Unajenga urafiki. Tafiti zinaonyesha asilimia 2% ya wateja hununua kwa mara ya kwanza na 98% hununua baada ya kufuatiliwa. Hii ni kwa sababu ya urafiki. Na watu wanapenda kununua kwa marafiki zao.
Nne; Ufuatiliaji unasaidia kupata mrejesho wa ubora wa huduma/ bidhaa au ubaya. Kumbuka ni asilimia 4% tu unayosikia kwa watu wasioridhika na bidhaa yako.

Ukomo wa ufuatiliaji;
Ufuatiliaji kwa mteja hauna ukomo kwani wateja wana watu wa karibu yao. Watakula, Watatembea, Watavaa, Watatumia simu, Wataibiwa na kutumia vifaa tofauti maisha yao yote. Wasipotumia wao. Kuna watu wao wa karibu. Kazi ya muuzaji ni kumfanya mteja asisahau biashara.

Muhimu; Mambo matano ya kutoka nayo:

Moja; Tenga muda wa kuwafuatilia wateja kila siku.
Mbili; Andaa orodha ya wateja wa kufuatilia.
Tatu; Andaa kitu cha kuwatumia au kuongea nao. Usiwapumzikie wateja. Wape kilichobora ili waendelee kuwa karibu yako.
Je, unafuatilia wateja wako?
Fanyia kazi yote ukiyojifunza katika makala hii.
Kwa mafundisho zaidi pata kitabu Cha MAUZO NI HUDUMA Ndani yake kimeelezea mengi kuhusu namna ya kuwafuatilia wateja, kuomba rufaa na kuwabakiza Katika biashara yako milele. Ni wewe tu kuchukua kitabu hicho kwa ajili ya kupata maarifa zaidi.

Makala imeandaliwa na Lackius Robert, Mwandishi wa vitabu na Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo. Karibu tuwasiliane kupitia 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz

Hakika, mauzo ni huduma.
Karibu tujifunze na kuuza zaidi
Karibuni.

Leave a comment