Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Sifa Kuu Tatu Za Ukamilishaji Kwenye Mauzo

Habari njema muuzaji bora kuwahi kutokea,

Hatuwezi kupata kile tunachotaka kwenye maisha yetu pasipo ukamilishaji.
Ukamilishaji ni hatua ya mwisho ya lengo lolote ambalo mtu anakuwa anafanyia kazi.

Kumbe basi, ukamilishaji ndiyo unaoleta ushindi. Na kwenye ukamilishaji kila mtu anakuwa anaondoka na ushindi.

Na ukamilishaji ni mchezo wa kubadilishana ushindi.
Kila mtu anakuwa anapata ushindi fulani kwenye ukamilishaji wowote ule.
Kwenye ukamilishaji wa mauzo, anayeuza anapata ushindi wa fedha na anayenunua anapata ushindi wa bidhaa au huduma aliyonunua.

Kifupi, ukamilishaji ni kitendo cha kumtenganisha mteja na fedha zake. Na kwa sababu watu wamepata fedha zao kwa shida, inapofikia kwenye kutoa hela huwa kunauma.
Ndiyo maana mnaweza kukubaliana na mtu kwamba akipata fedha, atakupa lakini akipata anakuwa hakupi, anahisi kuumia.

Kwenye mchezo wa mauzo, bila ukamilishaji hakuna chochote kikubwa kitakachotokea kwenye biashara. Ukamilisaji ndiyo unaleta kila kitu kwenye biashara.

Na mteja unakuwa umemkamilisha pale anapokuwa amekupa fedha na siyo sababu. Kwa mfano, mteja akikuambia nitakutafuta nikiwa tayari, jua hapo bado hujaweza kumkamilisha.

Ushindi unahesabika pale wewe umeishika fedha ya mteja au umeiweka mfukoni. Kama hujamtenganisha mteja na fedha zake, kazi ya ukamilishaji inakuwa haijafanyika.

Kwenye jumatano yetu ya leo ya ukamilishaji, tukiongozwa na kauli mbiu yetu; ABC: ALWAYS BE CLOSING- MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA.

Kwenye makala yetu ya leo, tunakwenda kujifunza sifa kuu tatu za ukamilishaji.

Moja ni kujitoa hasa yaani commitment.
Mauzo ni vita. Ila vita isiyoruhusu kumwaga damu.
Ili ukamilishe mauzo unapaswa kuwa mtu ambaye umejitoa kweli kwenye kile unachouza.

Mbili ni msimamo yaani consistency.
Bila kuwa na msimamo, huwezi kukamilisha mauzo.
Watu ni wagumu na wabishi kwenye kutoa hela, licha ya kuwa na njia zenye ushawishi bila kuwa na ung’ang’anizi mauzo yatakuwa magumu kwako.

Siyo tu mteja akikuambia hapana na wewe umwambie basi sawa. Hapana, pambana na endelea kumfuatilia na kumshawishi mpaka anunue.
Mpe manufuu ambayo atakwenda kunufaika nayo bila kuacha kwa msimamo na mauzo yatakuwa rahisi kwako.

Tatu ni mtazamo wa uwezekano.
Kumbuka, unakuwa kile unachofikiria.
Ukiamini unaweza, utaweza kweli. Na ukiamini huwezi na hutaweza kweli.

Mchezo mzima uko kwenye mtazamo wako. Hakikisha mara zote unakuwa na mtazamo chanya kwenye kila mauzo unayofanya.

Ona uwezekano na utaona milango ya mauzo inafunguka na utauza mpaka utashangaa.

Njia rahisi ya kujifunga kwenye mauzo inaanzia hapa kwenye mtazamo wako. Chunga sana mtazamo wako, kwa sababu ndiyo unaounda na kubomoa vitu.

Hatua ya kuchukua leo;

Moja ni kuwa mtu wa kujitoa hasa kwenye kila ukamilishaji wa mauzo.

Mbili ni kuwa mtu wa msimamo, usikate tamaa mpaka ukamilishe mauzo.
Usiishie njiani mpaka ufikie mwisho na mwisho wako ni kuweka hela mfukoni.
Kamwe usikubali juhudi zako unazoweka ukaziacha ziende bure bila ushindi.

Tatu ni kuwa na mtazamo wa uwezekano.
Hapa ndiyo mahali ufunguo ulipo.
Kwenye kila mauzo unayofanya, amini unakwenda kukamilisha mauzo na kumtenganisha mteja na fedha zake.

Sina uhakika kama itakufaa lakini ukiweza kujitoa hasa, ukawa na msimamo na mtazamo chanya kwenye mauzo, lazima utafanikiwa.

Nenda ukayafanyie kazi haya na kesho uje utupatie ushuhuda wako.

Kauli mbiu yetu; ABC: ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA.

Mwl.Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz

1 Comment

  • Miraji abdallah
    Posted November 8, 2023 at 3:40 pm

    Ktk makala hii nimetambua kwamba mchezo mzima wa mauzo unaanzia ktk mtazamo wa muuzaji.
    Unapaswa kuwa na mtazamo chanya
    ona uwezekano wa mauzo kukamilika.
    mirango yote ya mauzo itafunguka na utafanya mauzo mengi yatakayokushangaza.
    Hatua ninazokwenda kuchukua ni kufanya mazoezi kabla ya kukutana na mteja , kwani mauzo ni vita , lakini ni vita isiyoluhusu umwagikaji wa damu .
    Ushindi halisi ni ule mteja ananufaika na bidhaa au huduma aliyoipata na muuzaji ananufaika na mauzo pia faida aliyopata kupitia mauzo.

Leave a comment