Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Mbinu Mbili Za Ukamilishaji Wa Mauzo-3-4

Habari njema wauzaji bora kuwahi kutokea,

Karibu sana katika jumatano yetu ya ukamilishaji na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.

Kipimo cha ushindi kwenye mchezo wowote ule ni magoli yaliyofungwa na siyo chenga.

Kwenye mchezo wetu wa mauzo ushindi ni pale mteja anapotoa hela yake na kununua bidhaa au huduma anayotoa.

Pale unapomtenganisha mteja na fedha zake ndiyo ushindi wenyewe kwenye mauzo.

Jukumu lako kubwa kama mtu wa mauzo ni kumsaidia mteja kufanya maamuzi kwa mbinu za ukamilishaji kama tunavyokwenda kujifunza hapa.

Leo tunakwenda kujifunza njia mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo.

3. Ukamilishaji wa kipimo cha 1 mpaka 10

Kwenye ukamilishaji huu, unamwambia mteja 
“Kwenye kipimo cha 1 mpaka kumi, unaipa alama ngapi _ yako?” (Subiria jibu), akishakupa, uliza; “Nini kifanyike ili uipe alama 10?” (subiri jibu), akishajibu mwambie; “Vizuri, wacha nikamikishe hilo, kinachofuata baada ya hapa ni wewe kukamilisha malipo ili uondoke na bidhaa yako.

Ufafanuzi; huu ni ukamilishaji wenye nguvu na unaokuonyesha mtu anakikubali kitu kwa kiasi gani. Hata kama atakupa namba ya chini, usione kwamba hajakubali, ndiyo maana unamwuliza nini kifanyike ili ifike alama 10.

4.  Ukamilishaji wa bei kabla ya malipo.

Unamwambia mteja, “Tukubaliane kwanza kwenye bei kabla hujawa na wasiwasi kuhusu kukamilisha malipo. Hutaweza kujua kuhusu malipo kama hatujakubaliana bei.

unamwambia mteja tukamilishe hili la bei hapa ili tuendelee na mpango wa malipo.”

Ufafanuzi; ukamilishaji huu unamwondolea mteja sababu za kusubiri kwa kisingizio cha malipo. Unamfanya mkubaliane kwenye bei kwanza kisha ndiyo aendelee na mpango wa malipo.

Lengo kubwa la mbinu hizi, ni kujua kama mteja unayemuuzia ana uhitaji wa kile unachomuuzia au la.
Kwa kumwambia mtu tukubaliane kwanza bei kisaikolojia akikubali maana yake anakitaka kweli hicho kitu mpaka amekubali kwenye bei hivyo unakuwa unaongeza juhudi zaidi ili kumkamilisha.

Hatua ya kuchukua leo; nenda kazitumie mbinu hizi kwenye kukamilisha wateja kisha uje kutoa mrejesho wa kila mbinu unayotumia imekusaidiaje.

Kumbuka, mara zote unapaswa kukamilisha wateja, kwani kukamilisha ndiyo kuna leta fedha kwenye biashara yako.

Mwl.Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz

Leave a comment