Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Kifaa Kinachotuunganisha Katika Kujenga Mahusiano Na Wateja

Pata picha una mpenzi wako ambaye yuko Iringa na wewe uko Dar na kuonana na mpenzi wako ni mpaka wakati wa likizo tu.
Utajisikiaje kukaa na mpenzi wako kwa muda mrefu hivyo bila kuwasiliana naye mpaka mje kuonana wakati wa likizo?

Na kama unavyojua, ni hali ya hatari sana kwa mtu ambaye mnahusiana katika mapenzi halafu hakuna njia nyingine ya mawasiliano mpaka mkutane ana kwa ana wakati wa likizo.

Na kadiri utakavyomuacha mpenzi wako kwa muda mrefu bila mawasiliano ndivyo mahusiano yenu yanavyopungua na kupoteza nguvu. Waswahili wanasema, fimbo ya mbali haiui nyoka, hii ina maana kwamba mtu ambaye yuko mbali na wewe hawezi kuwa na msaada ila yule ambaye yuko karibu na wewe ndiyo ana ushawishi mkubwa sana kuliko mtu wa mbali.

Vivyo hivyo kwa mteja wako, yule ambaye uko naye karibu ni rahisi sana kumshawishi na kukubaliana na wewe kuliko yule ambaye yuko mbali.

Habari njema ni kwamba, kifo kifaa ambacho kinaweza kutuunganisha na watu wetu ambao tuko nao kwenye mahusiano ila wako mbali na sisi. Huenda mke, mume wako, mteja wako yuko mbali na wewe, lakini mnaweza kuunganishwa na kitu kimoja tu.

Sina uhakika kama itakufaa lakini kifaa ambacho kinaweza kutuunganisha pamoja na kujenga mahusiano yetu hata kama tuko mbali na wale ambao tunahusiana nao ni simu.

Tuko katika zama za taarifa, na kifaa ambacho kinatuunganisha sisi wote kwa pamoja ni simu.
Simu imekuwa ndiyo zana kuu ya mawasiliano katika zama hizi.

Kwenye CHUO CHA MAUZO, tunaumia simu kama zana kuu ya mauzo. Iwe mteja awe mbali au karibu kupiga simu kwa mteja ni lazima.

Mteja ni kama mpenzi wako, unapaswa kumpigia simu na kutaka kujua anaendeleaje.

Mpigie simu mteja kutaka kujua bidhaa uliyomuuzia, imekuwa na manufaa gani kwake, je, mteja anafurahia kile ambacho umemuuzia?

Mpigie simu mteja kumshukuru kwa manunuzi aliyofanya. Kama mteja wako alinunua leo, unapaswa kumpigia simu ili kumfuatilia kujua kama maendeleo ya kile ambacho umemuuzia.

Mpigie simu mteja na kumsalimia na kutaka kujua yeye anaendeleaje, familia yake, biashara yake.

Unapokuwa unamfikiria mteja mara nyingi, ndivyo na yeye anavyokuwa anakufikiria.

Hapa tunajifunza kwamba, mauzo ni mahusiano, wale ambao tunahusiana nao kwa karibu ndiyo wanakuwa watu wetu wa kwanza kununua kile ambacho tunauza. Haijalishi unajua nini, bali unamjua nani. Watu ambao unawajua ndiyo wanakuwa mtaji wako namba moja kwenye mauzo.

Hata wewe ukitaka kitu leo, hutaenda kununua kwa mtu usiyemjua, bali utaenda kununua kwa mtu unayemjua.

Mauzo ni mahusiano, huwa tunajisikia vizuri pale ambapo tunanunua kwa watu ambao tunawajua, kwa sababu tunawaamini, hivyo tunakuwa hatuna shaka yoyote juu yao. Ila tunaponunua kwa mtu tusiye mjua, tunakuwa na wasiwasi sana.

Ili wateja wako wasiwe na wasiwasi na wewe, unapaswa kuwa karibu na wateja wako. Unapaswa kujenga mahusiano bora na wateja wako kiasi kwamba hata wakitaka kwenda kununua, hawana mtu mwingine wanayemfikiria zaidi yako. Wafanye wateja wako wajisikie vizuri kununua kwako na pale wanapotaka kununua kwa mwingine, basi wajisikie vibaya, ili watu waendelee kununua kwako wanahitaji kuweka katika mchakato endelea wa mahusiano.

Na mauzo ni mahusiano, hivyo husiana vizuri na wateja wako na pale wanapokuwa na uhitaji wa kununua basi wanakuja kwako.

Habari njema ni kwamba, tumekuandalia kitabu kizuri cha MAUZO NI MAHUSIANO, anza kuweka oda yako mapema, na watakaoweka oda yao mapema, watapata zawadi.  Hii siyo ya kukosa, kwani ni kitabu ambacho kitakusaidia jinsi ya kujenga mahusiano bora na wateja wako.

Hatua ya kuchukua leo; weka oda yako mapema ili uwe wa kwanza kupata ofa na zawadi yako.

Kitu kimoja zaidi, mauzo ni mahusiano, mauzo siyo kitu cha siku moja, mauzo ni mchakato endelevu. Tunaohusiana na wateja wetu, basi jua kwamba tunahusiana nao daima. Kila mmoja ataendelea kumtegemea mtu wake mpaka pale kifo kitakapowatenganisha hata ikitokea kifo, basi wale watu wetu wa karibu bado tunaweza kuendelea kuhusiana na kufanya biashara.

Mwisho, mauzo ni njia sahihi ya kuweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako. Mauzo ndiyo ushindi wa uhakika, ukipata umepata, hivyo usipange kukosa kusoma kitabu hiko, siyo tu kitakusaidia sana kwenye mauzo, bali pia kuboresha mahusiano yako, utakuja kunishukuru baadaye baada ya kukisoma kitabu hiko.

Naomba unisaidie kitu kidogo, naomba unisaidie kuisambaza makala hii kwa mtu wako mmoja tu unayempenda ambaye unataka naye aje kunufaika kama utakavyonufaika wewe na kitabu cha MAUZO NI MAHUSIANO.

Kutoka kwa rafiki na muuzaji mwenzako,
CIO, Mwl Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa Chuo Cha Mauzo,
Barua pepe; makamu@mauzo.tz
Simu; 0717101505 wasapu na kawaida/0767101504.
http://www.t.me/chuochamauzo
www.mauzo.tz

2 Comments

  • Linda
    Posted August 23, 2023 at 10:07 am

    Nmejifunza vyema mauzo ni mahusiano

Leave a comment