Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Jinsi Ya Kutumia Silaha Ya Tano Ya Ushawishi Ya MAMLAKA Kufanya Mauzo Zaidi

Habari njema muuzaji bora kuwahi kutokea,

Mpaka sasa tumeshajifunza silaha za ushawishi ya fadhila na msimamo na kwenye kulipa fadhila tukaona jinsi mtu anavyotoa kidogo na kukitumia kupata makubwa zaidi.

Kwenye msimamo tukaona jinsi mtu akishawishika kufanya kitu kidogo, atakubali kufanya kikubwa baadaye.

Kwenye kufuata mkumbo, tukajifunza jinsi kufuata mkumbo kunavyowasukuma watu kufanya vitu ambavyo peke yao wasingefanya.

Na kwenye kupendeza tuliona jinsi wale wanaotaka kushawishi, wanamfanya mtu awapende wao kwanza na akishawapenda anakubaliana na kile anachowashawishi.

Baada ya kupata utangulizi kuhusu silaha za nyuma, kinachofuata baada ya hapa ni kujifunza silaha ya tano ya ushawishi ambayo ni MAMLAKA (AUTHORITY)

Kwenye silaha hii ya MAMLAKA, huwa tunawasikiliza na kuwaamini wale ambao wamepewa MAMLAKA fulani.
Kwa mfano, kama daktari amekuambia kitu fulani kuhusu afya yako, unamsikiliza na kuamini kwa sababu ana MAMLAKA kwenye eneo hilo la afya.

Confident African male leader standing telling diverse colleagues about new project, boss lead briefing for different age workgroup team employees in office. Sharing information and leadership concept

Hata kwenye mauzo, wewe kama muuzaji, mteja anakusikiliza pale unapokuwa unajiamini na kuijua biashara yako na unapompendekezea kitu, anakuona wewe kama ni mtaalamu wa mauzo.
Kama unauza halafu hujui biashara yako, watu watakupuuza kwa sababu wanakuona huna mamlaka.

Tokea tunazaliwa tumekuwa chini ya mamlaka ya wazazi, mpaka tunakua bado tunakua chini ya mamlaka fulani na tumelelewa kutii mamlaka.

Na tumeona kwa jinsi gani mtu usipotii mamlaka kunavyoleta madhara makubwa kwa mfano, Adam na Eva walikiuka maagizo ya Mungu na kula tunda walilokatazwa na kupelekea kufukuzwa kwenye bustani ya Edeni.

Kifupi, tumekuwa chini ya mamlaka maisha yetu yote.
Kuanzia utoto mpaka hali ya utu uzima bado tuko chini ya mamlaka.
Kwa mfano, kwenye taaluma unakuwa chini ya mamlaka ya ngazi ya juu ya kitaaluma na hata kwenye jamii, bado kwa ujumla tuko chini ya mamlaka mbalimbali ya viongozi wa kiserikali, kidini, na kijamii.

Kama muuzaji igiza kama mtu mwenye mamlaka pale unapouza kile unachouza iwe ni huduma au bidhaa.
Pia, vaa kama vile mtu mwenye mamlaka kiasi cha mteja kukuamini na kukubaliana na wewe kirahisi.

Ukitaka kuwashawishi watu kupitia silaha hii, tumia alama zifuatazo;

Moja ni vyeo.
Wewe kama muuzaji, ukitaka watu wakubaliane na wewe kirahisi jipe cheo fulani na watu watakuamini na kukubaliana na wewe. Kwa mfano, mteja anapokuwa anaongea na wewe, pale mwanzoni mnapokutana hata kwa wasakaji unapotembelea biashara, ukifika kule, jipe cheo.
Kwa mfano, jitambulishe wewe kama meneja masoko na mauzo, mkurugenzi nk.
Kitendo cha wateja kusikia kwamba wewe ni mkuu wa kitu fulani, tayari wanakuwa na ile hali ya kutii mamlaka na kukusikiliza na kukupa umakini.

Mbili ni mavazi.
Mavazi huwa yanaibua sana utii wa mamlaka fulani ndani yetu.
Kwa mfano, ukikutana na mtu amevalia sare ya polisi, moja kwa moja utatii mamlaka hata kama siyo polisi kweli.

Tumia mavazi ya juu, yanamuonesha mtu mwenye hadhi ya juu kama vile suti au sare za kampuni. Kitendo cha kuvaa sare ya kampuni, mteja anajua wewe ni mtu mwenye mamlaka hapo unapouza.

Tatu ni Vito vya Thamani.
Huwa tunakubaliana na watu ambao wanavaa na kutumia vitu vyenye thamani kubwa kama vile magari ya kifahari, mikufu ya madini ya ghali, saa za bei kubwa na nk.

Kama unataka kumshawishi mtu kwenye mauzo na watu kukuamini na kukubaliana na wewe ukitumia vito vya thamani, watu wanakuamini na kukubaliana kirahisi na wewe.
Mfano, matapeli wengi wanatumia njia hii ya kutumia Vito vya Thamani kukamilisha utapeli wao.

Watu wanatumia vito vya thamani kwa sababu wanajua watu wa vitu vya thamani hawawezi kuwatapeli na hivyo wanajikuta kushawishika na kutapeliwa kweli.
Kwa mfano, mtu anayetaka kwenda kuomba zabuni fulani kwenye taasisi, anaenda akiwa amevaa vizuri na kutumia Vito vya Thamani kiasi kwamba wale wenye zabuni waone huyo mtu yuko vizuri kweli.

Mwl.Deogratius Kessy
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz

Leave a comment