Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Mfumo Wa Mauzo Na Namna Unavyokupa Umiliki Wa Biashara

Mfumo Wa Mauzo ni jukwaa la ambalo huhifadhi taarifa muhimu na maelezo ya wateja ili kuwafuatilia kwa kina. Jukwaa hili husaidia kampuni na timu nzima ya mauzo kuwafuatilia wateja kwa ukaribu hatimaye kuwabadilisha kuwa wateja kamili. Mfumo huu wa mauzo unaongozwa na kitu kinachoitwa “Customer Relationship Management”(CRM). Taarifa hizi zinaweza kuhifadhiwa kwenye Google Sheet, Excel, Mchakato Mauzo au nyingine.

Ndani ya CRM kunakuwa na orodha ya taarifa za wateja. Ambapo taarifa hizo ndizo biashara hutumia kumfuatilia mteja hadi kumkamilisha. Baadhi ya taarifa muhimu kuweka kwenye mfumo wa kuwafuatilia wateja CRM ni kama;

_Jina la mteja
_Jina la kampuni
_Tarehe ya kuingia kwenye mfumo
_Hali ya mteja (tarajiwa au kamili)
_Barua pepe
_Ushabiki wake na taarifa nyinginezo kuhusu mteja husika.

Madhumuni Makuu Ya Kutumia Mfumo Katika Mauzo ni;

Moja; Kuwachambua Wateja.
Hii inakupa urahisi wakati wa kuwasiliana nao. Pia, unajua sehemu ya kuweka mteja anafaa kutembelewa, kutumiwa ujumbe au kupigiwa simu.

Mbili; Kuwashawishi Wateja.
Baada ya kuwachambua kinachofuata ni kuwashawishi kununua. Hapa hutumii nguvu kubwa kama mwanzo maana kuna baadhi ya taarifa unakuwa umepata.

Tatu: Kuwakamilisha Wateja.
Mara baada ya uwasilishaji wako mbele ya mteja hatua inayofuata ni ukamilishaji. Hapa unatumia mbinu kama ya kudhania, “summary”, na zingine nyingi kufanya mteja anunue.

Umuhimu wa Kutumia Mfumo Katika Mauzo;

Moja; Huanzii sifuri.
Unakuwa na mahali pa kuanzia maana taarifa za mteja unakuwa umezijaza. Unatumia taarifa hizo wakati wa mazungumzo na mteja.

Mbili; Ukaribu na mteja.
Hii ni baada ya kuwa na baadhi ya taarifa zake muhimu. Kama jina ambalo ni sauti wanayopenda kusikia wengi.

Tatu; Kutoa Huduma Bora.
Hii ni kwa sababu unakuwa unajua maendeleo na hali ya mteja kama ni kamili au tarajiwa. Unampa huduma nzuri kama kumshauri, kumsikiliza na zingine nyingi.

Nne; Kukamilisha Wateja.
Kuwa na mfumo wa mauzo ni sawa na chakula kinachopikwa jikoni. Muda wowote kinaweza kuiva, kutokana na aina ya moto uliopo kwenye chungu. Kupitia kuwatumia ujumbe mfupi, kuwapigia au kuwatembelea unajikuta umemkamilisha mteja.

Tano; Kuwajua Wateja Wako(Kumiliki biashara)
Hii ni kupitia orodha ya majina na taarifa unayokuwa nayo kwenye mfumo. Unajua fulani kanunua au bado.

Sita; Kuongeza Ufanisi Kwenye Mauzo.
Hii ni kwa sababu hata biashara ikibadili muuzaji taarifa za mteja zitakuwepo kwenye “database”. Hali inayofanya muuzaji mpya kucheza na taarifa hizo, badala ya kuanza upya.

Muhimu; Hakikisha unahifadhi taarifa za mteja sahihi kwenye mfumo wako. Usahihi wa taarifa kama jina lake na kampuni ndio hufanya mazungumzo na mteja kuwa mepesi.

Kwa hayo na mengine mengi usikose kutufuatilia hapa hapa. Unaweza kuchukua vitabu vyetu vya mauzo au kujiunga kwenye program ya Chuo Cha Mauzo. Lengo ni kuungana na wewe katika safari ya kukuza biashara yako na kuongeza mauzo angalau mara mbili.

Imeandaliwa na Lackius Robert, Mkufunzi Wa Mauzo na Mwandishi. Tuwasiliane 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz . Tufuatilie www.mauzo.tz

1 Comment

  • Faraji
    Posted December 14, 2023 at 6:00 am

    Kumbukumbu za wateja ni moja ya silaha muhimu katika mauzo

Leave a comment