Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Karibu CHUO CHA MAUZO.

CHUO CHA MAUZO ni programu ya mafunzo kwa watu wa mauzo yenye lengo la kuwafanya kuwa wauzaji bora.

Ni programu yenye mafunzo ya nadharia na vitendo ambayo yanagusa maeneo yote muhimu ya mauzo ili kumjengea muuzaji ujuzi bora wa mauzo utakaomwezesha kufanya mauzo makubwa.

Programu hii ina urefu wa mwaka mmoja (wiki 50) ambapo kuna mafunzo ya kila wiki, hatua za kuchukua kila siku na ripoti za kutoa kila siku na kila wiki. Mafunzo ya kila wiki yanakuwa ni ya kukutana ana kwa ana au kwa njia ya mtandao.

Mkakati mkuu wa programu ya CHUO CHA MAUZO ni kubadili MTAZAMO, kutoa MAFUNZO sahihi ya mauzo na kutoa MOTISHA wa kuwasukuma wauzaji kujituma zaidi kwenye mauzo.

Matokeo yanayotegemewa kwenye programu ya mauzo ni mauzo kuweza kukua mara mbili au zaidi ndani ya mwaka mmoja.

Leave a comment