Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Jinsi Kukaa Kwenye Mchakato Sahihi Kunavyowanufaisha Wauzaji

Mchakato wa mauzo ni mfululizo wa shughuli zote zinazofanyika na muuzaji ili kuweza kuwakamilisha wateja. Shughuli hizo ni kama kupiga simu, kufuatilia wateja za zingine nyingi.

Ili uweze kukaa kwenye mchakato lazima uwe na malengo. Dhumuni la malengo ni kukupa hamasa na  mwelekeo kulingana na shughuli unazofanya.

Kuwa na malengo ya siku, wiki, mwezi na mwaka. Ndiyo huchagiza ufanisi wa mchakato wako. Maana ni ngumu kukaa kwenye mchakato bila kuwa na miongozo sahihi. Na miongozo hii inategemea uwepo wa malengo.

Unapoweka malengo na kuanza kuyafanyia kazi ndipo watu husema unafanya kazi vizuri sana. Maana namba zinakuwa zinaonyesha.

Ukikaa kwenye mchakato na kufanya kazi kwa usahihi kufanikiwa ni suala linalowezekana kabisa.

Mambo ya kuzingatia ili ukae kwenye mchakato kwa usahihi;

Moja; Jua unachotaka na unakoenda.
Napoleon Hill aliwahi kunukuliwa akisema; “dunia ina tabia ya kutoa nafasi kwa mtu ambaye maneno yake na matendo yake yanaonesha anajua wapi anapokwenda”.

Mbili; Acha tabia ya Ughairishaji.

Tatu; Epuka makosa madogo madogo kutawala katika eneo lako.

Nne; Kuwa mkweli mara zote. Mtu pekee anayesema ukweli ni kinyozi. Maana huachi kichwa kwenye saluni yake.

Tano; Waheshimu Watu wote. Heshima haina gharama.

Sita; Kuwa mtu wa kufanya mara zote.

Kanuni ya siku 90 inasema; Shughuli zote zinazofanyika ndani ya siku 30 matokeo yake huonekana kuanzia siku ya 90. Kama muuzaji unayetaka kuuza zaidi lazima ukae kwenye mchakato sahihi na kufanya yaliyo muhimu.

Saba; Kuwa mvumilivu.

Mauzo mara zote sio tukio bali ni kitu cha muda mrefu. Sio rahisi umpate mteja leo umuuzie, wengine wanahitaji ufuatiliaji wa muda mrefu.

Hadi hapo, tayari umeishajua mambo ya kuzingatia, umeweka malengo yako, unajua unakoenda, mauzo unayotaka kupata, wateja tarajiwa, kamili na rufaa. Kazi kwako ni kukaa kwenye mchakato sahihi na kuongeza juhudi.

Kumbuka; Unaweza kudanganya kwenye kufanya, lakini matokeo yakakukamata.

Unaweza kusema biashara yangu biashara yangu inaendelea vizuri. Lakini namba za biashara, zikakukamata.

Usiigize maisha ndugu yangu. Ishi vile unavyotaka na unavyoweza usiruke ngazi. Nenda taratibu. Pole pole ndiyo mwendo.

Hatua ya kuchukua leo; Kuwa mkweli kwenye maisha na utendaji wako. Kuwa mwaminifu mara zote. Kaa kwenye mchakato kweli na usiigize maisha. Muda ukifika chochote kile unachotaka kwenye maisha yako, utakipata kama kweli umejitoa kukifanyia kazi na kukaa kwenye mchakato sahihi.

Kwa hayo na mengine mengi usikose kutufuatilia hapa hapa, kuchukua vitabu vyetu na kujiunga kwenye program ya Chuo Cha Mauzo. Ili ukuze biashara yako.

Imeandaliwa na Lackius Robert Mkufunzi Wa Mauzo na Mwandishi.
Tuwasiliane 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz

Leave a comment